WALIOANZISHA MAKAZI KIHOLELA KATIKA HIFADHI ZA MISITU MKOANI KATAVI KUONDOLEWA KWA NGUVU,WAKUU WA WILAYA WAPEWA RUNGU NA MKUU WA MKOA
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Raphael Mugoya Muhuga akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake(Hawapo pichani)(PICHA NA.Issack Gerald) Agosti 3,2016 |
Waandishi wa habari Mkoani Katavi wakiwa katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 3,2016 |
Na.Issack Gerald Bathromeo
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral
Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga ametoa agizo wa wakazi Mkoani Katavi wanaoishi
katika hifadhi za wanyama,misitu ya hifadhi na maeneo yasiyo rasmi kuondoka
wenyewe kwa hiari kabla ya kuondolewa kwa nguvu.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati
akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake ambapo amesema ametoa agizo
hilo ili kunusuru misitu inayoendelea kuteketea kutokana na uanzishwaji wa
makazi mapya na ufyekaji miti ovyo.
Aidha Jenerali Muhuga kabla ya
kuzungumza na waandishi wa habari,amefanya kikao na wakuu wa Wilaya zote tatu
za Mkoa wa Katavi na kuwaagiza kusimamia zoezi la kuwaondo wavamizi wa misitu
na kuharibu Mazingira.
Hata hivyo amesema wakala wa kuhifadhi
misitu Mkoani Katavi wana changamoto ya uhaba wa watumishi ambapo mpaka sasa
kuna watumishi 21 kati ya 250 wanaohitajika na hivyo zoezi la kupambana na
waharibifu wa mazingira na misitu kuwa migumu kwa kuwa hata vyombo vya usafiri
hawana.
Wakati huo huo amesema mpaka sasa kuna
kesi mbili zinazohusishwa na uharibifu ambapo katoi ya hizo kesi moja ni ya
Afisa mtendaji wa katika serikali za mitaa aliyeruhusu watu kufyeka miti na
kuanzisha makazi holela na kupelekea uharibifu wa mazingira.
Katika hatua nyingine,Mkuu wa Mkoa
amekitangaza Kijiji cha Majalila kilichopo kata
ya Tongwe kuwa makao makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Mhariri: Issack Gerald
Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments