WAKUU WA IDARA ZA ARDHI MKOANI MWANZA OFISINI HAPAKALIKI,JINO KWA JINO KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI
Na.Albert Kavano-Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongera Leo
amezindua program ya kushughulikia Migogoro ya ardhi mkoani humo na
kuagiza wakuu wa idara ya ardhi kutotoka nje ya wilaya wala kuingia
ofisini siku ya jumanne badala yake wakae na kutatua migogoro hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw.John Mongera |
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mkoa huo kuwa na
migogoro ya ardhi isiyo malizika kutokana na utata wa umiliki wa ardhi kwa
wananchi wa mkoa wa Mwanza hali inayo sababaisha wengi kuzungukia ofisi za mkuu
wa mkoa na wakuu wa wilaya kwa matatizo ya ardhi.
Katika uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja
vya hamashauri ya jiji Bw Mongera amesema kuwa katika malalamiko kumi sita ni
ya ardhi, hivyo wakuu wa idara watatakiwa kufunga ofisi na kutafuta eneo ili
kuwasikiliza na kushughulikia migogoro hiyo kabla ya kuwajibishwa wenyewe.
Aidha amewataka wananchi kuepuka tabia za
utapeli wa kugushi nyaraka za umiliki wa ardhi na atakaye kuwa na nyaraka
bandia atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Mhariri: Issack Gerald
Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments