MKUU WA MKOA WA KATAVI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO



Na.Issack Gerald Bathromeo
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga leo anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari.
Taarifa ya kikao hicho baina ya Mkuu wa Mkoa na waandishi wa habari,imetolewa jana na katibu wa mkuu wa Mkoa wa Katavi Bw.Philipo Charles.
Mkuu wa Mkoa qwa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga
                           

Hata hivyo Bw.Cahrles hakubainisha licha ya kusema kikao hicho kinatarajia kufanyika majira ya saa sita mchana,hakubainisha madhumuni ya kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral mstaafu Raphael Mugoya Muhuga amekuwa na utamaduni wa kukutana na waandishi wa habari anapohitaji kutoa taarifa za mkoa wa Katavi kuzungumza na wananchi Mkoani Katavi.
Kikao cha Mwisho baina ya Mkuu wa Mkoa na waandishi wa Habari kilihusu Uanzishwaji wa benki wa Benki ya wananchi Mkoani Katavi kikao ambacho kilifanyika wiki iliyopita katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA