WAKAZI KIJIJI CHA ITENKA KUANZA UJENZI KITUO CHA POLISI
Na.Issack Gerald Bathromeo
Wakazi wa Kijiji cha Itenka kilichopo
Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wametangaza kuanza
ujenzi wa kituo cha Polisi katika kijiji hicho.
Baadhi ya akina mama katika mkutano wa kijiji(PICHA NA.Issack Gerald) |
Taarifa ya mchakato wa ujenzi wa
kituo cha polisi kijijini hapo,imetolewa na mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Marco
Katambi wakati wa mahojiano na waandishi wa habari katika makao makuu ya kijiji
hicho yaliyopo hapo Itenka.
Aidha Bw.Kitambi amesema,kwa muda
Mrefu,kijiji cha Itenka hakina ulinzi imara ambapo askari huonekana tu siku ya
mnada kuimarisha usalama katika mnada uliopo katika kijiji hicho.
Baadhi ya wananchi wameiomba serikali
kongeza nguvu zaidi katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa wao wapo tayari
kuchangia asilimia 20 wanazotakiwa kuchangia katika ujenzi wa maendeleo.
Mbali na kijiji hicho kutokuwa na
kituo cha Polisi,wananchi pia wanasema wanakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa
maji safi na salama,huduma za afya,shule,miundombinu ya barabara na ukosefu wa
stendi kwa ajili ya maegesho ya magaari na pikipiki.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments