WALIMU NA WATENDAJI WA KATA WILAYANI KIBONDO WATAKIWA KUKOMESHA UTORO WA WANAFUNZI
Walimu wa shule za msingi na
watendaji wa kata Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma amewataka kuhakikisha kuwa
wanafunzi wanaacha utoro na kuhudhuria shuleni bila kukosa.
Moja ya shule zilizopo wilayani Kibondo Mkoani Kigoma |
Wito huo umetolewa na Afisa elimu
Shule za msingi Wilayani Kibondo Bw
Joseph Ntirutangwa wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake.
Aidha Bw.Ntirutangwa amesema viongozi
wa madhehebu wanatakiwa kutoa wito kwa waumini wao ili kuwahamasisha watoto wao
kuhudhuria shule waepukane na kitendo cha kuwafanyisha kazi kwa muda wanaopaswa
kuwa shuleni kusoma.
Mara kadhaa wazazi wamekuwa
wakilaumiwa uwatumikisha shamani watoto wao na kujikuta watoto hao wanafanya
vibaya katika mitihani wanayofanya.
Hata hivyo hali ya ufaulu wa
wanafunzi katika Wilaya ya Kibondo siyo nzuri katika takwimu za ufaulu wa
wanafunzi katika mitihani ya taifa.
Mwandishi:Jastin Cosmas=Kibondo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments