AHUKUMIWA MIEZI 9 AKIDAIWA KUTOROKA AKIWA CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI WILAYANI MPANDA
Mahakama ya mwanzo mjini Mpanda
imemhukumu mtu mmoja mkazi wa kata ya Misunkumilo kifungo cha miezi tisa jela
kwa kosa la kutoroka akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi.
Akisoma hukumu hiyo,hakimu mwandamizi
wa Mahakama hiyo Mh.David Mbembela amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Mohamedi Hamdany (24) ambaye alidaiwa kutenda kosa
hilo Julai 7 mwaka huu usiku katika
kituo cha polisi Mpanda mjini.
Aidha imedaiwa kuwa Bw.Hamdany
alikuwa anakabiliwa na kesi nyingine ya wizi wa pikipiki ambapo aliamua kutoroka
akiogopa kupelekwa mahabusu ambapo alitoroka baada ya kuvua pingu aliyokuwa
amefugwa mkononi na kukimbia kuelekea maeneo ya mtaa wa madukani .
Makosa ya watuhumiwa kutoroka chini
ya ulinzi yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara wilayani Mpanda.
Kwa mjibu wa mahakama, mtuhumiwa amefungwa kifungo hicho ili iwe
fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Katika hatua nyingine,Sanjari mtu mwingine
anaefahamika kwa jina la Michael Damas (40) mkazi wa Tambukareli kata ya Mpanda
Hotel amefikisshwa mahakamani kwa tuhuma ya kosa la kuchoma moto nyumba .
Akisoma shitaka hilo mwendesha
mashitaka wa jeshi la polisi CP Mtei amesema Bw.Damas alitenda kosa hilo Desemba
19 mwaka 2015 ambapo aliteketeza nyumba
na vitu vyote vilivyokuwa ndani vyenye thamani ya kiasi cha shilingi
laki tano na elfu kumi na nne mali ya Anatalia Gulionkondwe.
Kwa upande wake mshitakiwa amekana
kutenda kosa hilo na kesi hiyo imehairishwa hadi itakapo tajwa tena Julai 27
mwaka huu kwa ajili utetezi upande wa mshitakiwa
Comments