MANISPAA YA MPANDA YAANDAMWA ZAIDI NA MAAMBUKIZI YA VVU,KATAVI NAYO NDANI YA MIKOA 10 BORA YENYE VVU NA UKIMWI
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
imeendelea kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya Ukimwi na kuchangia Mkoa wa
Katavi kuendelea kuwa miongoni mwa mikoa 10 ya Tanzania yenye maambukizi hayo.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha
Wadu wa kupambana na maambukizi ya VVU na Ukimwi ambacho kimefanyika Manispaa
ya Mpanda.
Mratibu wa Ukimwi katika Manispaa ya
Mpanda Bi.Mary Byaro amesema kikao hicho kimewakutanisha kujadili mikakati ya
kupambana na maambukizi ya Ugonjwa huo katika Manispaa ya Mpanda.
Kikao hicho kimeshirikisha wadau
mbalimbali wa kupambana na VVU na Ukimwi wakiwemo Waratibu wa Ukimwi Mkoa wa
Katavi,Manispaa ya Mpanda,viongozi wa dini,wazee,vijana na asasi za kiraia
ikiwemo SHDEPHA.
Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2014,asilimia 6 ya watu waliopima VVU
waligundulika na VVU ambao kwa uwiano watu 16 mmoja aligundulika kuwa na
maambukizi ya VVU hii ni kwa jinsi zote
Aidha mwaka 2014 maambukizi yanayohusisha
wanawake Wajawazito yalikuwa ni 4% ya
waliopima VVU kwa uwiano wa watu 23 ambapo katika idadi hiyo mjamzito mmoja
alikutwa na maambukizi.
Katika hatua nyingine Takwimu za mwaka
2015 zinaonyesha waliogundulika na
maambukizi kati ya waliopima ni 4% kwa uwiano wa watu 23.
Katika uwiano wa wanawake 21 mmoja
alikutwa na maambukizi,kwa uwiano wa wanaume 23 mmoja aligundulikana maambukizi
huku wa uwiano wa wajawazito 23 waliopima,mmoja alikutwa na maambukizi.
Wakati huo huo katika mahudhurio ya
Kliniki mwaka 2014 takwimu
zinaonyesha 28% ya wenza walihudhuria
kliniki ya wajawazito na kupima VVU kwa pamoja huku mwaka 2015 47% ya wenza walipima VVU kwa pamoja na kupelekea ongezeko la hudhurio la wanaume
kwenye klininik ya wajawazito
Aidha Takwimu zinaonyesha kuwa watoto
waliozaliwa na akina mama wenye VVU 99%
walipimwa maambukizi kwa miaka yote
miwili 2014 na 2015 ambapo 6% ya watoto waliopima waligundulika na maambukizi
ya VVU
Hata hivyo kwa mjibu wa taarifa ya
waratibu wa Ukimwi Manispaa ya Mpanda,changamoto zilizopo katika kupambana na
Ukimwi ni pamoja na Ufinyu wa maeneo ya kutolea huduma,Ushiriki mdogo wa
wanaume ,Uhaba wa vitendanishi,Ongezeko la watoro wanaotakiwa kupata huduma,Usafiri
usio wa uhakika kwenye shughuli za
huduma mkoba,Ukosefu wa kiyoyozi maabara,Wafadhili kuendelea kujitoa kusaidia
huduma mbalimbali ikiwemo ununuzi wa madawa
(septrine) matengenezo ya
vifaa nk
Hata hivyo,licha ya Manispaa ya
Mpanda kupambana na changamoto mbalimbali za kukabiliana Ukimwi wameendelea
kuweka mikakati ikiwa ni,kuongeza siku za huduma,Kushirikiana na watoa huduma wa magonjwa majumbani wa taasisi
ya (SHIDEFA) ,expert na mama mwam bata
kuwatafuta,Kuongeza vituo vya tiba na matunzo,Ukarabati wa chumba kwa shughuli
za maabara ,Bajeti ya ununuzi wa madawa.
Kwa
upande wake Mratibu wa TACAIDS Mkoani Katavi Bw.Yahya Mussa Mumbaga amesema Kiwango
cha maambukizi ya VVU katika Mkoa wa Katavi ni asilimia 5.9%,Rukwa asilimia 6.2%,Kigoma
asilimia 3.4 na Tabora asilimia 5.1%.
Halikadhalika katika tafiti zilizofanyika mwaka 2011-2012 kiwango cha
maambukizi ya VVU kwa wanaume na wanawake wenye umri wa miaka 15-49 nchini
Tanzania,Takwimu zinaonesha kuwa kwa ujumla maambukizi kwa Tanzania
yamefikia 5.1%,Tanzania bara 5.3% na Tanzania
visiwani chini ya 1%.
Maambukizi ya VVU yako
juu sana katika mikoa ya Njombe (14.8%), Iringa (9.1%) na Mbeya (9.0%) huku mikoa yenye Maambukizi ya chini ikiwa ni mikoa ya Pemba (0.3%), Unguja (1.2%) na
Lindi (2.9%)
Baadhi
ya njia kuu zinazopelekea maambukizi ya VVU na Ukimwi Ngono zembe,kushirikiana
katika matumizi ya vitu vyenye ncha kali ikiwa miongoni mwao kuna mwenye
maambukizi,Ubakaji,kuongezewa damu ya mtu mwenye maambukizi ya VVU,mapenzi ya
jinsia moja na kutotumia kinga au mpira ujulikanao kama kondomu wakati wa
kujamiana.
Na
njia za kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi ni kuepuka hizo njia ambazo
zimetajwa kusababisha maambukizi.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments