POLISI WAKAMATA PEMBE ZA NDOVU 666.
Mkurugenzi wa idara ya jinai Bw.Diwani Athumani, amesema
kuwa wageni wawili ni miongoni mwa watu 9 waliokamatwa katika operesheni hiyo.
Operesheni hiyo iliyohusisha maafisa wa polisi wa kimataifa
kutoka Harare,Zimbabwe na Nairobi Kenya ilifanikiwa kupata genge la watu 43.
''operesheni ‘Usalama III’ ilianza juni tarehe 26 hadi tarehe
30 na ilihusisha maafisa kutoka mataifa 26 barani Afrika waliokuwa na jukumu la
kupeleleza na kunasa genge lililohusika na uwindaji haramu''. alisema Athumani.
''Tulifanikiwa kuwanasa walanguzi hao pamoja na wawindaji
haramu 256 pamoja na bidhaa zao zilizotengenezwa kwa pembe za ndovu''
Vile vile tulifaulu kukamata mihadarati kama vile heroine,
bhangi, miraa mbali na silaha kali ikiwemo bunduki 12 na risasi 104'' alisema
bwana Athumani.
''tutatoa bidhaa hizi zote kama sehemu ya ushahidi wa polisi
mahakamani aliongezea kusema bw Athumani.
Athumani aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
kuwa washukiwa watafikishwa mahakamani karibuni.
Comments