WAKAZI KIJIJI CHA KAKESE MANISPAA YA MPANDA WAELMISHWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI
WAKAZI wa
kijiji cha Mbugani kata ya Kakese Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameaswa
kutunza vyanzo vya maji vilivyopo bonde la Mto Mpanda.
Picha na p5 tanzania |
Picha na P5 tanzania |
Rai hiyo
imetolewa leo na Afisa Maendeleo ya
Jamii Tadeus Ndeseiyo wa idara ya maji na umwagiliaji bonde la ziwa Rukwa alipokuwa akitoa elimu katika mkutano wa
hadhara ambao umefanyika kijijini hapo.
Ndeseiyo
amezitaja changamoto zinazohatarisha mto Mpanda
kuwa ni shughuli za kilimo na umwagiliaji pamoja na uchungaji mifugo
unaoendelea pembezoni mwa mto huo.
Hata hivyo
baadhi ya wanakijiji wameeleza kutofahamu sheria ya kulima mita sitini kutoka mtoni ili kulinda vyanzo
vya maji hali ambayo elimu isipotolewa haraka kwa wananchi hawa huenda mto
katika miaka mitano ukawa umetoweka.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa
ambayo inakabiliwa na uharibifu wa mazingira hususani vyanzo vya maji.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack
Gerald Bathromeo
Habarika zaidi
na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments