MIRADI 9 YAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU MANISPAA YA MPANDA
ZAIDI ya miradi 9 ikiwemo Stendi Mpya ya kisasa ya mabasi katika
Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imezinduliwa leo.
Vijana wakimbiza mwenge wa uhuru(PICHA NA Issack Gerald) |
Miradi hiyo imezinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Bw.George
Jakson ambapo amesema miradi hiyo itasaidia kukuza maendeleo ya jamii pamoja na
uchumi wa mkoa.
Baadhi ya wananchi walioshiliki katika uzinduzi wa miradi hiyo wamesema
wanashukuru kwa kuzinduliwa kwa miradi hiyo ambapo wameiomba serikali
kuwasaidia vifaa vya kisasa ili
kuboresha maendeleo yao kutokana na shughuli za kiuchumi wanazozifanya kila
siku.
Hata hivyo mwenge wa uhuru leo unakesha katika viwanja vya shule ya
msingi Kashato Manispaa ya Mpanda ambapo kesho unatarajia kuelekea katika
halimashauli ya mpya ya Tanganyika mkoani Katavi na hatimaye utakabidhiwa
Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments