MWENGE WA UHURU WAHITIMISHA MBIYO ZAKE WILAYANI MLELE WAZINDUA MIRADI,WAPOKELEWA MANISPAA YA MPANDA
WAKAZI
wa tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wametakiwa kutoziharibu
barabara za mitaani katika tarafa hiyo zilizotengenezwa kwa kiwango cha lami.
Rai
hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwnge wa Uhuru Kitaifa George Jackson
Mbigima wakati wa Uzinduzi wa barabara zenye urefu wa KM 2 sanjali na
Miradi mbalimbali katika Mbio za mwenge wilayani Mlele.
Ujenzi
wa barabara hizo umetekelezwa na kutumia bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016
ambapo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni 710 ambazo zilitengwa kwa ajili
ya utekelezaji wa mradi huo katika Halmshauri ya Wilaya ya Mlele.
Aidha
Mbigima ameiomba Halmashauri ya Mlele kuwawezesha vijana kukidhi vigezo vya kukopesheka
katika benki mbalimbali ili kuondokana na wimbi la kukaa vijiweni pasipo
kufanya kazi na kupelekea kufanya uharifu.
Awali
akiwasilisha taarifa hiyo Mhandisi wa Ujenzi Halmashauri ya Mlele Bw.Simioni
Lwitiko Kasumo amesema Ujenzi wa Mradi huo Umetekelezwa chini ya Mfuko wa
Barabara wa Halmashauri pamoja na nguvu ya wananchi.
Mwenge wa uhuru Umepokelewa katika Halmashauri ya
Wilaya ya Mlele mkoani Katavi ukitokea katika Halmashauri Mpya ya Mpimbwe baada
ya kupokelewa kutoka Mkoani Rukwa katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe Umezindua
Miradi Mbalimbali ndani ya wilaya ikiwemo Mradi wa Maji Utakaowezesha kupunguza
kero ya Maji kwa wakazi wa tarafa ya Inyonga.
Mwenge wa uhuru umewasili leo Halmshauri ya Manispaa
ya Mpanda kuendelea na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo
miradi ya maji,ujenzi wa barabara na vikundi vya kupambana na kuzuia Rushwa.
Mwenge wa uhuru ukiwa Mkoani Katavi unatembelea Jumla
ya Halmashauri 5 ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda,Mlele,Mpimbwe,Halmashauri
ya Wilaya ya Mpanda na Tanganyika.
Mbiyo za mwenge wa uhuru mkoani Katavi
zitahitimishwa Julai 14,2016 na kukabidhiwa Mkoani Kigoma kupitia wilaya ya
Uvinza.
Kauli
mbiyu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni ‘’Vijana ni nguvu kazi ya taifa,washirikishwe
na kuwezeshwa’’
Mwandishi:Ester Lameck
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments