RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA MPANGO WA UGAWAJI MADAWATI,MKOA WA KATAVI KATIKA MGAO AWAMU YA KWANZA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amezindua mpango wa ugawaji wa madawati yanayotengenezwa kutokana na
fedha zilizotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kubana
matumizi katika bajeti yake.
Kwa mjibu wa Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasilian,zinduzi
huo umefanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam ambapo Rais
Magufuli amekabidhi madawati 537 kwa mbunge wa jimbo la Ilala Mheshimiwa Mussa
Azan Zungu kwa niaba ya wabunge wa majimbo yote ya Tanzania Bara na Tanzania
Zanzibar ambayo yatagawiwa idadi hiyohiyo ya madawati kwa kila jimbo.
Madawati hayo 537 ni sehemu ya madawati 61,385 ambayo
yametengenezwa katika awamu ya kwanza na yatafuatiwa na madawati mengine 60,000
yatakayogawiwa katika awamu ya pili.
Madawati yote kwaujumla yanatarajia kugharimu shilingi
bilioni 4 ambazo zilitolewa na Bunge tarehe 11 Aprili, 2016 baada ya kubana
matumizi katika bajeti yake,ikiwa ni kuitikia wito wa Mhe. Rais John Pombe
Magufuli.
Mikoa itakayonufaika katika awamu ya kwanza ya ugawaji wa madawati
hayo ni Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Njombe,
Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Unguja, Pemba na Tanga.
Akizungumza katika hafla hiyo,Rais Magufuli amewashukuru na
kuwapongeza wabunge kwa kutoa mchango huo na pia amewapongeza wadau wengine
ambao wameitikia wito wake wa kuchangia madawati kwa lengo la kuondoa tatizo la
wanafunzi kukaa chini.
Rais Magufuli amesema baada ya kuanza kutekeleza ahadi ya
kuondoa ada kwa shule za msingi na sekondari,idadi ya wanafunzi waliojiandikisha
kuanza darasa la kwanza imeongezeka kutoka wanafunzi 1,282,100 hadi kufikia
wanafunzi 1,896,584 sawa na ongezeko la asilimia 84.5 hali iliyosababisha
upungufu wa madawati 1,400,000 lakini tatizo hilo limetatuliwa kwa kiasi
kikubwa ambapo mpaka sasa zaidi ya madawati 1,000,000 yametengenezwa.
Aidha, Dkt. Magufuli amelitaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
na Jeshi la Magereza kuongeza kasi katika utengenezaji wa madawati ili
yakamilike haraka na kuanza kutumika.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson,Wabunge wa kamati ndogo ya tume ya huduma za
bunge,Viongozi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Magereza pamoja
na wanafunzi wa shule ya msingi Bunge.
Chanzo:Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ya Rais
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments