WAFANYABIASHARA WAILALAMIKIA SERIKALI KUWAZUIA KUTEKELEZA HAPA KAZI TU,WANGOA MABANGO USIKU WA MANANE WAKIPINGA KUFUKUZWA ENEO LA KIBIASHARA
Na.Issack Gerald
Bathromeo-Katavi
Wafanyabiashara wadogo waliopo genge
la kufanyia biashara lililopo Mtaa na Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi wamelalamikia uongozi wa serikali ya Mtaa,kata ya Mpanda Hotel na
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa kutowapatia eneo maalumu la kufanyia
biashara huku wakifukuzwa katika kila eneo wanalokwenda kufanyia biasahara.
Bango lililong'olewa na kutupwa kusikojulikana katika genge la biashara lililopo mtaa na kata ya Mpanda hotel lililopigwa marufuku(PICHA NA.Issack Gerald) |
Wafanyabiasahara wadogo wakiwa katika genge wakiuza bidhaa zao katika genge lililopigwa marufuku(PICHA NA.Issack Gerald) |
Genge jipya eneo la mtaa wa Mpanda ana Kata ya Mpanda Hotel lililopigwa marufuku(PICHA NA.Issack Gerald) |
Wakizungumza kwa jazba na hasira
katika genge hilo,wafanyabiasaha hao zaidi ya 300 sasa,wamesema kuwa wamechoshwa
na usumbufu wanaoupata katika uongozi wa serikali hizo na wanachokitaka sasa ni
kurudishiwa fedha yao au kupelekwa katika eneo lingine lililo karibu na makazi
yao ambapo tofauti na hapo wataomba msaada zaidi ngazi zinazofuata.
Wamesema kuwa katika eneo ambalo
walitimuliwa tangu Julai 24,viwanja wanavyouzia biashara hizo walipimiwa na
kugawiwa kwa gharama ya shilingi 10,000/= kila mfanyabiashara ambapo hatua hiyo
imewashangaza na kuwaumiza kuonekana kuwa hawana haki wakati viwanja hivyo
walipewa na serikali ya mtaa na kata inayotambulika kisheria.
Mpaka sasa wamehamishwa na kufukuza
katika maeneo matano kuanzia mwaka 2015 ambapo katika eneo la kwanza la karibu
na machinjio ya Mpanda hotel walitimuliwa kwa madai kuwa watakanyagwa na
ng’ombe na pia siyo eneo halali la soko.
Maeneo mengine waliyotimuliwa wafanyabiashra
hao ni pembezoni mwa barabara iendayo Mkoani Kigoma kuanzia Mpanda na katika
maeneo ya viwanja vya watu binafsi huku wanapotimuliwa ikiwa hakuna
wanapooneshwa wanakotakiwa kupelekwa kufanya biashara zao katika mitaa yao.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw.Alfred
Mtaita akitolea ufafanuzi wa suala hilo amesema,wananchi wapo eneo hilo
kihalali kwa kuwa eneo hilo siyo mali ya Idara ya ujenzi Halmshauri ya Wilaya
ya Mpanda wanaodai eneo hilo kuwa mali yao wakati ni Chama cha Mapinduzi kata ya Mpanda Hotel.
Hata hivyo kwa upande wake Diwani wa
Kata hiyo Mh.Willium Liwali ambaye naye anahusishwa na wafanyabiashara
kuwaruhusu kutumia eneo hilo,amewataka kuendelea na biashara zao kama kawaida
wakati mazungumzo ya kuleta suluhu yakifanyiwa kazi ili kuondoa mgogoro wa ummiliki
halali kati ya Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda na Chama cha Mapinduzi kata ya
Mpanda Hoteli.
Wakati huo huo Siku ya
Jumapili,mabango 3 kati ya 4 yaliyokuwa yamesimikwa katika viwanja hivyo
yaling’olewa na kutupwa kusikojulina na watu wasiojulikana na hiyo ikiwa ni
ishara ya wafanyabiashara hao kutokubaliana na aliyeweka bango hilo.
Jumla ya Shilingi miloni moja laki
saba na na elfu hamsini (1,750,000/) zilikwishachangwa na wafanyabishara na
kiasi cha fedha tayari kimetumika kujenga choo katika eneo hilo ambapo mgogoro
huo umezuka rasmi tangu wiki iliyopita baada ya wafanyabiashara kuanza biashara
zao.
Miongoni mwa bidhaa zinazouzwa katika
genge hilo ni pamoja na mbogmboga,matunda,viazi na mitumba ya nguo.
Mapema mwaka huu,Waziri Mkuu wa
Tanzania Mh.Kassim Majiliwa aliziagiza Halmshauri zote nchini kutenga maeneo ya
uwekezaji.
Comments