WAZIRI MASHA NA WENZAKE 9 WASHINDA KESI MAHAKAMA YA WILAYA YA MPANDA,KATIBU CHADEMA WILAYA YA MPANDA ASISITIZA KUANZISHA MASHTAKA DHIDI YA WALIOWASUMBUA.
NA.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Aliyecchuchumaa chini ni Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Lawreance Masha(PICHA NA.Issack Gerald Katavi |
Mahakama ya
Wilaya ya Mpanda jana imewaachia huru washtakiwa 10 akiwemo aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana Mwanza Mh.Lawrence Kego Masha baada ya
mahakama kutowakuta na hatia katika makosa waliyokuwa wakishtakiwa.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari kuhusu kesi hiyo,Katibu wa Chama cha Demokrasia
Wilayani Mpanda Bw.Iddy Omary Faraji amethibitisha kuachiwa huru kwa viongozi
wake 10 akiwemo pia Mgombea ubunge jimbo la Nsimbo mwaka 2015 Bw.Gerald Kitabu.
Waziri Masha
na wenzake na Viongozi tisa wa Chadema Mkoani Katavi kutoka Jimbo la Nsimbo na
Mpanda Mjini,walikuwa wakishtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni Kula Njama Ili
Kutenda Kosa na Kuhutubia Wakimbizi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2015 na kosa lingine likiwa la kuingia makazi ya Wakimbizi bila Kibali.
Mahakama imesema,upande wa mwendesha mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wowote unaonyesha kwamba washtakiwa hao walikutana na kupanga njama kutenda kosa huku pia kukiwa hakuna ushahidi wowote kuonyesha kwamba washtakiwa walikamatwa wakihutubia wakimbizi.

Mahakama
iliwataka Washtakiwa walitakiwa kujibu shtaka la kuingia kwenye kambi/makazi ya
wakimbizi bila kibali ambapo Mara baada ya uamuzi huo washtakiwa walitakiwa
kutoa utetezi wao ambapo washtakiwa Lawrence Masha na Stansalaus Kaswele
walitoa utetezi wakiongozwa na Wakili Albert Msando.
Baada ya Mahakama kusikiliza utetezi ndipo mahakama ikatoa hukumu na kusema kuwa washtakiwa wote saba hawana hatia kwa kukubaliana na hoja zote za Wakili wa Utetezina hivyo washtakiwa wako huru.
Baada ya Mahakama kusikiliza utetezi ndipo mahakama ikatoa hukumu na kusema kuwa washtakiwa wote saba hawana hatia kwa kukubaliana na hoja zote za Wakili wa Utetezina hivyo washtakiwa wako huru.
Hata hivyo
Katibu Iddy Omary Faraji amesema kuwa baada ya kushinda kesi,kinachofanyika
sasa ni kuangalia namna ya kufungua shtaka kutokana na usumbufu walioupata kwa
kipindi chote cha kesi huku wakiwa hawana hatia.
Aidha
amewataka wananchi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuwa
watuliwa na kusisitiza kuwa hawatakubaliana na vitendo vyote vya unyanyasaji na
kusisitiza kutumia mihimiri ya sheria kutafuta haki.
kutafuta haki.
Comments