MIRADI 71 ILIZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
Bathromeo-Katavi
Jumla ya Miradi 71 ya maendeleo
ilizinduliwa katika Mkoa wa Katavi huku baadhi ya miradi hiyo ikiwa katika
sekta ya elimu,kupambana na rushwa,ujenzi wa Miundombinu ya barabara na afya.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga wakati akizungumza
na waandishi wa habari Ofisini kwake.
Alisema kuwa katika miradi hiyo yote
iliyokaguliwa na mwenge wa Uhuru ina thamani ya Shilingi Bilioni 16.3.
Aidha alitoa shukrani kwa wakazi wa
Mkoa wa Katavi kwa kuonesha hali ya amani na utulivu katika kipindi chote cha
mbio za mwenge wa uhuru ulipokuwa Mkoani Katavi.
Mwenge wa uhuru ulianza mbio zake
Mkoani Katavi Julai 10 hadi 14 ukitokea Mkoani Rukwa na Julai 15 kupokelewa
katika Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.
Kauli mbiyu mwaka huu inasema ‘’Vijana ni nguvu kazi ya taifa,washirikishwe
na wawezeshwe’’
Comments