LEO WAZIRI MKUU PINDA MGENI RASMI TUZO ZA WALIMU KATAVI
Na.Issack Gerald Bathromeo
Leo Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda
inatarajia kutoa tuzo za kuwapongeza walimu wa shule za msingi zilizopo Manispaa
ya Mpanda Mkoani Katavi baada ya kufaulisha Wanafunzi kwa ufaulu wa asilimia 90
hadi 97 kwa mwaka 2014 na 2015 na kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwa miaka
miwili mfululizo kwa kufaulisha wanafunzi.
Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda(PICHA NA.Issack Gerald |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Mpanda Bw.Michael Fransis Nzyungu amsema kuwa mgeni rasmi katika hafla hii
anatarajia kuwa Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Mh.Mizengo
Kayanza Peter Pinda.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga amesema kuwa walimu hao
wanatakiwa kupatiwa pongezi kwa kuwa wameleta heshima kubwa katika taifa hili
la Tanzania kuanzia mwaka 2013 tangu ulipoanzishwa mpango wa Matokeo Makubwa
sasa.
Mwanzoni mwa wiki hii,Mkuu wa idara
ya elimu shule za msingi(Afisa elimu) Bw.Visent Kayombo alisema kuwa ufaulu kwa
mwaka 2013 ulikuwa asilimia zaidi ya 62,2014 asilimia 90 na 2015 asilimia 97
ambapo hata hivyo akasema kuwa kulingana na mikakati iliyopo kwa sasa
wanatarajia kufaulisha kwa asilimia 98 katika mitihani itakayofanyika 2016.
Wakati huo katika ngazi ya Mkoa,mkoa
wa Katavi katika matokeo ya mtihani kwa mwaka 2014 ulishika nafasi ya tatu na
2015 kushika nafasi ya kwanza kwa kufaulisha wanafunzi wa shule za msingi kwa
kiwango cha juu.
Hata hivyo manispaa ya Mpanda imekuwa
ikifanya vizuri pia katika sekta nyingine ambapo kwa miaka ya hivi karibuni
Manispaa ya Mpanda(Wakati huo hadhi ya mji) ilipata tuzo kwa kushika nafasi ya
kwanza kwa hapa nchini kwa kuwa mji msafi kuliko miji yote hapa nchini.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments