ZAIDI YA MATUKIO 27 YALIYOTIKISA KATAVI NA NJE YA KATAVI MWEZI MACHI 2016 NA P5 TANZANIA
WATU WATANO WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO YENYE TAMANI YA MIL.60,280,650/= KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI WILAYANI MLELE
Katika tukio la kwanza habari zilizotufikia Machi 4 mwaka huu,Jeshi la Polisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi lilimkamata Bw. Robert Nyakie(40) mkazi wa kijiji na Kata ya kanoge barabara ya tatu kwa tuhuma ya kukutwa na meno ya tembo kinyume na sheria.
Kamanda
Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed alisema,mtuhumiwa alitenda
kosa hilo mnamo Machi mosi mwaka huu katika kijiji cha kanoge barabara ya kwanza.
Aidha,ACP
Mohamed alisema,Bw.Nyakie akiwa alikamatwa na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye uzito wa
kilogramu 11.50 ambavyo thamani yake ni Shilingi milioni Ishirini na saba na
laki saba na Elfu hamsini ambapo kamanda alisema ni sawa na tembo mmoja
aliyeuawa.
Kamanda
Mohamed alisema harakati za kumpeleka mahakamani Mtuhumiwa huyo aliyekuwa
amevichimbia vipande hivyo nje karibu na ukuta wa nyumba yake,zilikuwa
zikiendelea ili kujibu tuhuma inayomkabili mara baada ya upelelezi kukamilika.
Hata
hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wananchi kutojihusisha
na shughuli haramu za ujangiri na biashara za nyara za serikali kwani ni uhalibifu wa rasilimali za taifa letu hasa
kwa manufaa ya vizazi vijavyo na pia
amesisitiza hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wote
wasiotii sheria pasipo kushurutishwa.
Katika
tukio la pili siku nne tu baada ya tukio hilo la kwanza la Machi 4,harakati za
Jeshi la polisi zilizaa matunda tena Machi 8 mwaka 2016 baada ya kuwatia mbaroni watu 4 kwa
tuhuma za kukutwa na vipande vitatu vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu
11 vyenye thamani ya shilingi
milioni 32,530,650/=ambayo ni sawa
na tembo 01 aliyeuawa.
Kamanda
msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed aliwataja watuhumiwa hao
kuwa ni Frank Koroneli (25) Adela Alex (23) Moris ezron (34) na Sedekia
Shadrack(38) ambao ni wote wakazi wa kijiji cha Nduwi kata ya Katumba Wilayani
Mlele.
ACP
Mohamed alisema,mnamo tarehe 05.03.2016 maeneo ya Msasani Kijiji cha Nduwi
Station Kata ya Katumba,Jeshi la Polisi likiwa katika doria walipata taarifa
toka kwa raia wema kuwa katika Kijiji cha Nduwi kuwa kuna wakazi wanajihusisha
na shughuli haramu za ujangili ambapo baada ya taarifa hiyo kupokelewa ndipo
walipofuatilia na kuweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na
vielelezo hivyo huku wakiwa wamevificha vipande hivyo kwenye kichaka.
Hata
hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ametoa wito kwa wananchi kutojihusisha
na shughuli haramu za ujangiri na biashara za nyara za serikali kwani ni uhalibifu wa rasilimali za taifa letu hasa
kwa manufaa ya vizazi vijavyo na amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria
zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wote wasiotii sheria pasipo kushurutishwa.
Suala
la watu kukamatwa na nyara za serikali
bado linaendelea kufukuta Mkoani Katavi kwa harakahara utadhani kuwa ni wahusika
kutoogopa mkono wa sheria huku inaonekana Msemo za Mwenzako akinyolewa zako tia
maji ukiwa umeshindwa kutimia.
Harakati
za Mpanda Radio zinaendelea ili kupata ukweli zaidi kujua zaidi wangapi
waliokuwa wakiwafanyiwa upelelezi na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na nyara za
serikali wamefikishwa mahakamani hususani mwezi machi mwaka 2016.
JERA MIAKA 20
Katika hatua nyingine Jumatano ya
wiki hii Machi 30 ,mwaka 2016,mahakama ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu
mtu mmoja kwenda jera miaka ishilini baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na nyama ya kiboko.
Akisoma
hukumu hakimu mkazi mfawizi wa mahakama hiyo Bw Chiganga Twengwa alimtaja
mtuhumiwa kuwa ni Ramadhani Majengo (66)
mkazi wa masigo wilaya ya Mlele.
Alisema
mnamo Mei 5 mwaka jana,mtuhumiwa
alikamwatwa na jeshi la polisi akiwa
na kilo 40 za nyama hiyo bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa wanyama
poli.
Kufuatia
hukumu hiyo,mahakama imetoa amri kwa jeshi la polisi kumkamata kwa nguvu mtuhumiwa kwa sababu ya kuluka dhamana .
Pia
mahakama imetoa hukumu hiyo kama
fundisho na onyo kali kwa watu wenye tabia
ya kuuwa wanyama poli bila kuwa na kibali cha serikali.
KATIKA HABARI ZA WIZI WA WATOTO MKOANI KATAVVVI NA MWANZA HALIKADHALIKA FEDHA KWA NJIA YA MTANDAO.
WAWILI WILAYANI MPANDA WAKAMATWA WAKITUHUMIWA KUIBA MTOTO
Na.Vumilia Abel
Tuanzie na hii
ya wizi wa watoto,Tukianzia Katavi
Machi
15 mwaka huu,serikali ya kijiji cha Ikaka kata ya Mnyagala Wilayani Mpanda
mkoani katavi kiliwakamata watu wawili wanaofahamika kwa majina ya Edefance
John na Januari Kisulo wote wakazi wa kijiji cha Isengule kata ya Ikola kwa tuhuma za wizi wa mtoto mwenyeumri wa
miaka 13.
Taarifa
ya kukamatwa kwa wezi hao ilibainishwa Machi 15 na Afisa mtendaji wa kijiji
hicho Bw. Bw.leonard Michael Mbogambi kupitia kikao cha hadhara
kilichwashirikisha wananchi kikilenga kujadili kusoma mapato na matumizi ya
mradi wa maji.
Aidha
mtendaji huyo alikuwa amesema kuwa watu hao waliokamatwa watapelekwa katika
vyombo vya sheria na ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.
Awali
mwenyekiti wa kijiji hicho B w.Mipawa Pikipiki alisema kuwa watu hao aliwapokea
majira ya saa 4 asubuhi wakiomba hifadhi ya kulala nyumbani kwake ili kesho
yake waendelee na safari ambapo hakufahamu kuwa mtoto waliyekuwa naye siyo wao.
Kwa
upande wake askari wa sungusungu wa kijiji hicho Bw.Fredy Nkana Tung’ombe
ametoa lawama kwa wazazi juu ya tukio kwa kutomtimiza mahitaji muhimu ya mtoto.
Kwa
kwa mujibu wa askari huyo, mtoto huyo ambaye hata hawezi kujieleza amekosa
mahitaji ya msingi ikiwemo elimu,mavazi na chakula.
Kwa
upande wa watuhumiwa,walikana kuiba mtoto ambapo walidai kuwa walifuatwa na
mtoto huyo baada ya kumwomba awaoneshe njia ya sehemu wanakoelekea.
Kwa
upande mama mzazi wa mtoto huyo Bi.Pascharia Valentino ambaye ni mkazi wa
kijiji cha Kalofesi alisema alikuwa akiishi na watu hao kwa mwezi mmoja mpaka kufikia
machi 15 mwaka huu.
Suala la tabia za watu wasiokuwa na
haya juu ya wizi wa watoto halikuishia Katavi pekee mwezi huu tuelekee mwanza
kuona nako hali ilikuwaje.
WIZI
WA MTOTO KUIBIWA MKOANI MWANZA MACHI 26,2016
Albert-Mwanza.
Mwanamke mmoja ambaye hakutambulika
maramoja anatafutwa na jeshi la polisi Mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga katika wodi
ya wazazi katika Hospitali ya wilaya ya
Magu na kutoweka naye kusiko julikana.
Tukio hilo limetokea Machi 23 mwaka
huu katika Hospitali ya wialaya Magu ambapo mwanamke mmoja ambaye hakutambulika
maramoja akiwa amevalia ushingi aliingia ndani ya wodi hiyo na kutoweka na
mtoto huyo.
Kamanda wa Polisi Mkao wa Mwanza
Justus Kamugisha ameeleza kuwa mwana mke
aliye ibwa mtoto ni Bi Magdarena Petro (16) na tukio hilo lilitokea akiwa usingizini
ikiwa ni siku moja tu baada ya kujifungua na Polisi mkoani humo inawahoji
Manesi, wauguzi na walinzi wa hospitali kwa tukio hilo.
Aidha Jeshi la polisi limeitaka jamii
kutoa taarifa ya mtu atakaye kuwa ame husika na wizi wa mtoto huyo na
akibainika atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.End’s
Matukio haya ya wizi wa watoto si
mara ya kwanza kuripotiwa hapa nchini na hakuna budi suala hili liangaliwe kwa
kina likianzia kwa jamii yenyewe kwa ujumla.
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, March
02, 2016
Na.Issack Gerald-Katavi
Katika
Mwezi Machi Mwaka huu kuliibuka sakata lililowahusisha wajasiliamali wakiwa
katika harakati za kutafuta maslahi baada ya Umoja wa wajasiliamali wa Pasifiki
waliopo mtaa wa majengo kata ya Kashaulili
pale umoja huo uliposhuhudiwa ukiilalamikia Manispaa ya Mpanda kwa kutoa
tenda ya kutengeneza madawati kwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Sailoni
Mwagama ambaye ni mjasiliamali wa eneo hilo tofauti na ilivyokuwa awali kuwa
wajasiliamali hao wangepata tenda hiyo kwa pamoja kama ilivyokuwa imetangazwa
na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw.Pazza Mwamlima.
Kutokana
na kuwa sakata hilo lilianza kufurukuta mwezi Februari,Machi 2 mwaka huu suala
hilo lilimbandua Ofisini Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na hatimaye kufika eneo hilo
la wajasiliamali kusuluhisha mgogoro huo wa kimaslahi.
Akitoa
ufafanuzi wa malalamiko hayo Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,katibu
tarafa wa Tarafa ya kashaulili Bw. Reginard Muhango katika mkutano
uliofanyika eneo hilo Machi 2, alifafanua
kuwa lengo na hadi ya mkuu wa wilaya ilikuwa ni kutoa tenda kwa kila mwana
pasifiki na si kwa mtu mmoja.
Wakati
Bw. Mhango akiwatoa wasiwasi wajasiliamali hao pia aliwaahidi kuwa huo siyo
mwisho wa tenda kufika mahali hapo.
Hata
hivyo katibu tarafa huyo alimuamru mwenyekiti wa umoja huo katika eneo la
Pasifiki,kugawa magogo kwa kila mjasiliamali ili kutengeneza madawati hayo.
Aidha
alitoa wito kwa wajasiliamali hao kuendelea na kazi kama kawaida pamoja na
kudumisha umoja kati yao na kuchangamkia fursa wanazopata ili kutengeneza vitu
vyenye ubora na ustadi wa hali ya juu.
Tenda
ya utengenezaji wa madawati kwa ajili ya Shule zilizopo Wilayani Mpanda
ilitangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mnamo Februari 27 mwaka 2016 ambapo
zaidi ya Magogo 130 yalitakiwa kugawanywa kwa wajasiliamali hao zaidi ya 300
badala yake kuchukuliwa na mtu mmoja hali ambayo ndiyo iliyosababisha hali ya
kutoelewana kwa wajasiliamali wenyewe na hatimaye Halmashauri ya Manispaa ya
Mpanda kulalamikiwa na kulazimika kuingilia kati.
Ukiangalia
hapa zilikuwa ni harakati za Manispaa ya Mpanda kuondoa tatizo la wanafunzi
kukaa chini kwa kigezo cha kukosa madawati.
Lakini
tukisalia katika suala la madawati ambapo tutasema kuwa ni neema kwa kiasi
Fulani ni pale Machi
24 mwaka huu,Wadu
mbalimbali wa elimu katika Manispaa ya Mpanda na halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda walipofanya harambee na kupata kiasi cha shilingi miloni 5 na elfu
65,madawati 224,mifuko 10 ya simenti na magogo 4 ya mbao kwea ajili ya
kutengeneza madawati.
Akizungumza
wakati wa harambee hiyo,mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Bw.Pazza Tusamale Mwamlia aliwapongeza wadau hao kwa michango hiyo na kuwaomba
kuendelea kuchangia kwa hiari.
Alisema
kuwa Jamii haina budi kuendelea kujitolea kuchangia madawati kwani kila suala
haliwezi kukamilika kwa kutegemea bajeti ya seriklai pekee.
Alisema
kuwa changamoto ya madawati kumetokana na ongezeko kubwa la wanafunzi
waliojiandikisha darasa la kwanza mwaka huu ambapo kwa kiwango cha juu baadhi
ya shule zimesajili wanafunzi hadi 800 kwa darasa la kwanza pekee.
Mkuu
wa Wilaya pamoja na kutoa shukrani kwa wadau waliojitokeza kufanikisha harambee
hiyo,pia aliitaka jamii kwa ujumla kuendelea kujitolea akisema kuwa kutegemea
pekee bajeti ya serikali haitoshi.
Akisoma
taarifa ya hali ya Mahitaji ya madawati katibu wa kamati ya kuratibu na
kutengeneza madawati Bw.Lukasi Sotel Nyambala alisema kuwa Halmshauri ya Wilaya
ya Mpanda ina upungufu wa madawati 8245 ambapo imetengeneza madawati 1500 huku
yanayohitajika kutengezwa yakiwa ni 7250 .
Kwa
upande wa Manispaa ya Mpanda Bw.Nyambala alisema kuwa Manispaa ina upungufu wa
madawati 5179 ambapo yaliyotengenezwa ni
554 huku yanayohitajika kutengenezwa yakiwa 4625.
Serikali
ya Tanzania ilisema matarajio ni ifikapo mwezi juni mwaka 2016 asiwepo
mwanafunzi atakayekaa chini kwa kisingizio cha kukosa dawati la kukalia.
Hata
hivyo kwa baadhi ya Halmshauri za Mkoa wa Katavi ikiwemo Manispaa katika
taarifa ya mapema mwezi Januari kufuatia agizo la serikali kutolewa likiwataka
wakurugenzi na viongozi wa ngazi za juu wa Mkoa wakitakiwa kutafuta ufumbuzi wa
tatizo la wanafunzi kukaa chini walisema watatoa taarifa ya mafanikio ya
utatuzi wa changamoto ya madawati ifikapo Machi 31.Kwa hiyo Maiki zetu
zitaelekea katika Ofisi za Halmshauri wakati wowote.
Na Mpaka Machi 30,mwaka 2016 taarifa ya Halmshauri
ya Wilaya ya Mpanda ni kuwa imeazimia kukamilisha agizo la serikali juu ya kutatua changamoto ya
upungufu wa madawati ifikapo May 30
mwaka huu.
Taarifa
ya mwandishi wetu Agness Mnubi ilibainisha kuwa Kaimu Mkurugezi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mpanda Kennedy Shilumba inaeleza kuwa wamejipanga kuhakikisha
ifikapo may 30 mwaka huu kuhakikisha wanakamilisha changamoto ya upungufu wa madawati katika shule za msingi
na Sekondari huku serikali ikitoa agizo kukamilisha zoezi hilo ifikapo juni 30
mwaka huu kama agizo la serikali kuu inavyoagiza.
Amesema
katika kukamilisha zoezi hili wameshilikisha viongozi mbalimbali pamoja na jamii
kwa ujumla.
Amefafanua
kuwa Mpaka sasa wamesambaza madawati
1250 na mahitaji ni 6287.
Pamoja
na kuiomba jamii kuendelea kushiriki katika kuchangia madawati anabainisha
zaidi.
Thursday,
3 March 2016
Katika
kikao hicho cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Katavi maarufu kama RCC kilichofanyika
Machi 3 katika Ukumbi wa Idara ya maji unaomilikiwa na Halmshauri ya Wilaya ya
Mpanda lakini ukiwa katika ardhi ya Manispaa ya Mpanda kililenga zaidi kujadili
masuala mbalimbali.
Kupitia
kikao hicho kilichomuhusisha Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya 10 katika
Serikali ya awamu ya Nne,Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda,Waziri Mkuu Pinda aliushauri
Mkoa wa Katavi kumaliza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji pia
katika maeneo ya makazi na hifadhi ambayo kwa miaka mingi imekuwa historia kwa
baadhi ya maeneo.
Alisema
migogoro ya ardhi inasababishwa na ongezeko la watu wanaohamia ndani ya mkoa wa
Katavi kutoka mikoa mingine nchini ikiwemo Shinyanga bila kufuata maelekezo ya
waraka wa serikali wa mwaka 2000.
Aidha
Waziri mkuu mstaafu Pianda alishauri mjadala huo upewe nafasi kubwa na kila
halmashauri mkoani Katavi itoe mwongozo wa matumizi ya ardhi na kutoa taarifa
katika ngazi ya mkoa ili ufumbuzi wa tatizo hilo upatikane.
Kikao
hicho kiliwashirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo mkoani Katavi wakiwemo
wabunge saba wakiwemo watano wanaochaguliwa na wananchi.
Migogoro
mingi katika Mkoa wa Katavi imekuwa ikiibuka ikihusisha wakulima na
wafugaji,maafisa kuuza kiwanja kwa mtu zaidi ya mmoja na wakulima kuingia
katika eneo la hifadhi za mkoa wa Katavi.
Friday,
4 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, March
04, 2016
Na.Meshack Ngumba-Katavi
Katika
hatua za Wanawake Mkoani Katavi kujinansua na hali ngumu ya kimaisha,Machi 4
mwaka huu walishauriwa kuunda Vikundi ili kupata fursa ya Kupewa misaada itakayowasaidia Kujikwamua Kimaisha
kwa kuanzisha Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Ushauri
huo ulitolewa na Mh,Taska Mbogo Mbunge Viti maalum Mkoa wa Katavi wakati wa
uzinduzi wa Vijiwe vya wanawake Katika kata za Uwanja wa ndege,Makanyagio na
Nsemulwa.
Katika
Uzinduzi huo Mh Mbogo alitoa Kiasi cha shilingi Milioni Moja na nusu kwa
vikundi vyote ili Kusaidia Uendeshaji wa Vikundi hivyo.
Wakizungumza
baada ya kupokea Msaada huo baadhi ya
akina mama waliohudhuria uzinduzi huo walipongeza juhudi za Mbunge zinazolenga
kuwatoa wanawake katika kundi la watu tegemezi katika jamii.
Mkoani
Katavi kumekuwepo vikundi mbalimbali vya wanawake wanaojishughulisha na kazi
mablimbali ikiwemo utengenezaji wa sabuni,ufumaji wa vitambaa huku wengine
wakijishughulisha na ufugaji licha ya kuwa hakuna soko la uhakika wanakoweza
kuuzia bidhaa zao.
Tuesday, 15 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, March
15, 2016
Na.Issack Gerald-Mpanda
Machi
15 mwaka huu,Watu wawili wakazi wa kijiji cha Ikaka kata ya Mnyagala wilayani Mpanda mkoani
Katavi,walifikishwa katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda wakikabiliwa na
shtaka la wizi wa fedha kwa njia ya simu
ambayo ni mali ya Charles Lubasha mkazi wa Kakese.
Akisoma
shtaka hilo mbele ya hakimu mwandamizi Bw David Mbembela,askari wa jeshi la
polisi WP8940 PC Shakira aliwataja
washtakiwa hao kuwa ni Bw.Emmanuel Makopo (23) na Cosmas Faustene(33)
waliotenda kosa hilo Machi 7 mwaka huu majira ya saa kumi jioni.
PC
Shakira alisema washtakiwa hao waliiba pesa zenye thamani ya shilingi laki sita
na elfu tano kwa kutumia simu mali ya Lubasha.
Na
matukio haya hayakukoma ambapo machi 30 mahakama ya Mwanzo Mjini Mpanda imefuta
kesi ya wizi wa kuaminiwa iliyokuwa ikimkabili Michael Maduhu (23) Mkazi wa
Karema .
Akifuta
kesi hiyo Hakimu Mkazi Sylivester Felix Makombe alisema Mtuhumiwa amefutiwa kesi
hiyo kutokana na mlalamikaji Hawa Hamis kutohudhuria Mahakamani.
Mshitakiwa
alifikishwa Mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa kutoaminiwa,ambapo mnamo
January, 22, 2016 alipewa fedha shilingi 90,000/=kwa lengo la kumpelekea mama
yake mlalamikaji na hatimaye mtuhumiwa akazitumia mwenyewe.
Tuesday,
8 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, March
08, 2016
Na.Issack Gerald-Mpanda
Machi
8 mwaka 2016,wanawake Mkoani Katavi,waliungana na wanawake wengine duniani
kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Katika
Wilaya ya Mpanda maadhimisho haya yalifanyika kwa kufanya usafi katika
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda wakiongozwa na Mbunge wa viti maalum mkoani Katavi
Mh.Anna Lupemmbe ili kuwasidia wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kufanya usafi.
Akizungumzia
siku ya Wanawake duniani,mbunge huyo alisema wanawake wamepiga hatua kubwa ya
kimaendeleo kutokana na kutambua umuhimu na nafasi yao katika jamii
Kwa
upande wao wanawake walieleza kufurahishwa
na maadhimisho hayo wakisema kuwa yamewawezesha kutafakari mchango wao katika
kuisaidia jamii kimaendeleo.
Siku
ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo machi 8 ambapo siku hii
hutumika kujadili masula yanayowahusu wanawake ikiwa ni pamoja na kujadili
namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.
Maadhimisho
haya ya mara ya 41 tangu umoja wa mataifa ulipotangaza rasmi kuanza maadhimisho
haya mwaka 1975 yanaongozwa na kauli mbiyu ya ‘’50-50 ifikapo 2030,tuongeze
jitihada’’.
Wednesday,
9 March 2016
KICHAPO KWA MADAKTARI NA WAUGUZI NA MADAKTARI KUTOKA
KWA WAGONJWA NA NDUGU WA WAGONJWA WATIKISA MWEZI MACHI SASA MIKOA YA
KATAVI,MWANZA NA MTWARA YAONGOZA.
Mwezi
ni mwezi mwaka 2016 ni mwezi ambao umefurika vituko na matukio ya kushangaza
yanayohusisha wagonjwa na ndugu wa wagonjwa kuwadunga makonde ya ngumi wauguzi.
Machi
8 mwaka 2016 mkoa wa Katavi ulianza kwa kushangaza umma pale uliposhudia Muuguzi Katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda akipigwa
na Mgonjwa aliyekuwa akimuhudumia huku serikali ikishauliwa Kuimarisha Usalama
wa watumishi Katika maeneo yao ya Kazi.
Katika
hali hiyo isiyokuwa ya kawaida imezoeleka kusikia wahuduma wa afya Katika vituo
mbalimbali hapa nchini wakilalamikiwa na wagonjwa Kwa Kutumia lugha zisizokuwa
na staha,lakini safari hii hali imekuwa tofauti
Kufuatia tukio la Mgonjwa Kumpiga ngumi Muuguzi wa zamu aliyekuwa
akimuhudumia Kwa Madai ya Muuguzi Kumtaka Mgojnwa huyo alale Kitanda Kimoja na
Mgonjwa Mwenzake.
Bi
Recho Matinya ambaye ni Muuguzi Katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambaye pia
ndiye Mwathirika wa tukio hilo alisema kuwa alipigwa ngumi,ambapo baada ya hali
hii ilimlazimu Muuguzi huyu kuiomba serikali Kukomesha matukio ya namna hii
Kutotokea tena kwa watumishi wengine wa
umma na pia Katika sekta nyingine.
Maria
Komba mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambapo kwa upande wake alilaani Kitendo
hicho na kuitaka Serikali kuangalia namna
ya Kulinda haki za wauguzi akisema kuwa mgonjwa huyo aliamka katika kitanda na
kumvagaa muuguzi.
Tukio
la muuguzi kupigwa ngumi lilitokea ikiwa ni takribani Wiki Moja kupita tangu
wabunge wa Viti Maalumu Mh,Anna Lupembe
na Mh Taska Mbogo Kutembelea Hospitali hiyo ili Kujionea Mapungufu yaliyopo
lakini hata kabla hawajaingia ndani Kulitokea Mvutano Kuhusu uhalali wa
Kufungwa kwa geti la Kuingia Katika hospitali hiyo Muda wote.
Hata
hivyo mgonjwa aliyempiga muuguzi alitokomea siku moja baada ya kumchalaza
muuguzi na hakujulikana alikoelekea.
Wakti
tukio hili likitokea hapa mkoani Katavi,Mkoani Mwanza wauguzi na madaktari katika Hospitali ya
Butimba wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza walilazimika kugoma
kutoa huduma kwa saa sita kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 6 mchana mpaka Mkuu wa
Wilaya ya Nyamagana alipoingilia kati suala hilo kwa madai mbalimbali likiwemo
madai ya kunyanyaswa na kutishwa na watu wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.
Hata hivyo mambo hayajakoma ikiwa ni mwendelezo wa
vijimambo vya mwezi machi kati ya Wauguzi/madaktari na wagonjwa wanaowahudumia
ambapo Machi 27 wauguzi na madaktari hatika Hospitali ya Rufani Ligula liyopo
Mkoani Mtwara nao pia waligoma kutoa huduma baada ya kudai
kuwa mwenzao amepigwa na ndugu wa mgonjwa hadi kuvuliwa nguo.
Tukio
la Daktari kupigwa lilitokea majira ya saa 11 asubuhi baada ya mgonjwa
aliyetokana na ajali ya pikipiki kulazwa hospitalini hapo tangu Jumamosi ya
Machi 26.
Hata
hivyo inadaiwa kuwa mgonjwa alimpiga daktari kwa madai ya kuchelesha kutibiwa
ambapo kwa upande wa daktari aliyepigwa Dk Sain Dickson alipigwa na mgonjwa
alipokuwa amekwenda kumwangalia mgonjwa baada ya kumwandikia vipimo vya X-ray
na kusema kuwa mgonjwa alikuwa akipatiwa matibabu.
Mpaka
kufikia Machi 28 mwaka huu kufuatia tukio la ndugu wa mgonjwa kumpiga Daktari
Mkoani Mtwara, tayari jeshi la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu wawili kwa kitendo hicho
cha kumpiga mganga wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.
Hatua ya kukamatwa kwa watu hao wawili kulithibitisha Machi 28
na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe akisema kuwa wathumiwa hao
wamekamatwa usiku wa kuamkia Machi 28 wakitaka kutoroka kuelekea nje ya nchi nchini
huku wengine watatu wakiendelea kusakwa.
Awali wauguzi na Madaktari wa Hospitali hiyo waligoma kufanya
kazi hadi hapo watakapohakikishiwa usalama wao ndipo wafanye kazi.
Machi 29,Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alifika Hospitalini hapo
na kusuluhisha mgogoro huo huku akiomba Jeshi la Polisi kuongeza usalama kwa
watumishi hao wa Afya.
Haya hali kwa sasa iko hivyo katika baadhi ya Hosptali zetu
Friday, 18 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, March
18, 2016
DAKTARI
wa zahanati ya Kapalamsenga wilayani Mpanda, aliyekuwa akituhumiwa na wakazi wa
kijiji hicho kusababisha kifo cha Bi.Anna
Kilangi (49) kwa kugoma kumhudumia, alijifungua salama mwanzoni mwezi Machi mwa
huu.
Kwa
mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mpanda ,Dk Jovin Mlinda alimtaja
daktari huyo kuwa ni Bi.Rehema Munga aliyejifungua mtoto mwenye uzito wa kilo
tatu hospitalini hapo Jumapili ya Machi 20,2016.
Siku
moja kabla ya kujifungua,askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka
kambi ya Ikola walilazimika kuilinda nyumba yake baada ya wananchi wenye hasira
kutishia kuichoma moto .
Bi
Anna Kilangi kabla ya kifo chake, alifikishwa katika zahanati hiyo saa moja
usiku kwa matibabu, lakini daktari huyo alikuwa tayari amelala nyumbani kwake,
na kutokana na hali ya ujauzito alishindwa kwenda kumhudumia mgonjwa huyo.
Matukio
ya madaktari kulalamikiwa kutotoa huduma kama inavyostahiri kwa wagonjwa yamekuwa yakitokea hata nje ya
mkoa wa Katavi ikiwemo Mkoani Mwanza.
Thursday,
10 March 2016
ZIARA
ZA WABUNGE WA KATAVI ZASHIKA KASI KATAVI,MBUNGE VITI MAALUMU ACHANGIA SOLA
KITUO CHA AFYA MPANDA
Kituo
cha afya cha Mwangaza kinachomilikwa na manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi
kimekuwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo kukosekana kwa vitendea kazi na kupelekea wagonjwa kukosa humuma
iliyo bora.
Hayo
yalibainishwa machi 10 mwaka huu na
wajumbe wa kamati ya bodi ya manispaa pamoja na wananchi waliohudhuria katika
ziara ya mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Bi.Roda Kunchela katika ziara
aliyoifanya kituoni hapo.
Walisema
kuwa wanahitaji umeme wa ziada ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa umeme unapokuwa umekatika.
Akijibu
na kutolea ufafanuzi changamoto hizo
Mh.Kunchela alisema amesikitishwa na suala la hali ya kituo hicho ambapo alijitolea
Sola kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.
Aidha
aliwaahidi kutatua changamoto ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka na kuwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa wito
ili kuhudumia jamii inayo wazunguka.
Mwezi
Machi ni mwezi ambao wabunge na madiwani walikuwa wakifanya ziara ya kusikiliza
kero za wananchi katika maeneo wanayoyatawala huku wananchi wakieleza kero zao
ili zipatiwe ufumbuzi kama waheshimiwa walivyoahidi.
Thursday,
10 March 2016
Machi
10 mwaka huu,Kamati ya kulea balaza la watoto wanaoishi katika mazingira magumu
yenye mradi ujulikano kama mradi wa elimu Jumuishi Wilayani Mpanda Mkoani
Katavi,walikutana na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuwasaidia
watoto wenye mahitaji maalumu.
Kwa
mjibu wa Mkurugenzi wa Shirika la IAS Tanzania Bi.Elizabert Mavoa ambaye alifanya
ziara mkoani Katavi na kuzungumza na kamati hiyo,alisema lengo la ziara yake ni
kupata taarifa mbalimbali ili kufahamu changamoto zinazowakabili watoto wenye
mahitaji maalumu katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Kwa
upande wake Mratibu wa mradi wa elimu Jumuishi
Tanzania Bi.Irene Shayo akaiasa kamati kushirikisha jamii na serikali
kutatua changamoto za watoto wenye ulemavu.
Naye
mratibu wa mradi wa elimu jumuishi katika mikoa ya Rukwa na Katavi Bw. Joseph
Ndomba alisema kuwa katika Mkoa wa Rukwa na Katavi tangu kuanzishwa kwa mradi
katika mikoa hii mwaka 2012,kuna mafanikio makubwa ikiwemo idadi ya wanafunzi
wenye ulemavu kuongezeka shuleni ili kupata elimu kama watoto wengine wasio walemavu.
Wakati
huo huo,katika kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto ya vitendea kazi,mradi wa
elimu jumuishi ulipatiwa zana mbalimbali ikiwemo gari na vifaa vingine ambapo
mradi huu hufanya kazi katika Wilaya za Mpanda,Nkasi na Sumbawanga.
Mradi
wa elimu Jumuishi wa awamu ya pili ulianza mwaka 2015 mbapo kila mradi hudumu
kwa kipindi cha miaka 3 kabla ya kusaini mkataba wa mradi mwingine.
Mpaka
sasa tangu mwaka 2012,mikoa pekee ya Katavi na Rukwa kati ya mikoa 30 ndiyo
mikoa iliyopewa kipaumbele kwa mradi wa elimu jumuishi hapa Tanzania.
Mwaka
2015,jumla ya wtoto 62 wenye mahitaji maalumu Wilayani Mpanda waliokuwa
hawapewi kipaumbele, waliibuliwa na kupelekwa kati shule mbalimbali kusoma
wakiwemo wawili wenye ulemavu wa ngozi Albino walipelekwa kusomea Sumbawanga
Rukwa.
Kamati
ya balaza la mradi wa elimu jumuishi Wilayani Mpanda,inafanya kazi chini ya
ufadhili wa mashirika matatu yaliyoungana na kuunda umoja wao unaojulikana kama
IFI.
Mashirika
haya ni International Aids
Services(IAS),Free Pentekoste Church Of Tanzania(FPCT) na International Center
Of Disabilities
Friday,
11 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, March
11, 2016
NA.Issack Gerald-Katavi
Machi
11 mwaka huu,Wafanyabiasha wa soko la Buzogwe wamelalamikia hatua ya kikosi cha
zima moto Manispaa ya Mpanda mkoani wa Katavi
kwa kuwatoza kodi ambayo haijulikani inakopelekwa pamoja na
kutoelimishwa juu ya michango hiyo.
Wakizungumza
katika mkutano ulioitishwa na uongozi wa soko hilo,wamesema kikosi hicho kinawatoza kodi ya Shilingi Elfu Arobaini.
Walisema
kuwa askari hao wamekuwa wakiwapa vitisho vya kuwapeleka mahakamani na kuonesha
ubaguzi kwa baadhi ya wafanyabiahara kuhusu kulipa kodi hiyo huku wengine
wakiwa hawalipi kabisa.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa soko hilo Bw. Ramadhani Karata alikiri askari hao
kuwatisha wafanyabiashara na kuwakuzia faini kwa wale ambao hawajalipa licha ya
kuwa hawana elimu kuhusu michango hiyo.
Akijibu
malalamiko hayo, Mkaguzi Mkuu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa katavi
Kamanda Edward Kakwale alisema,kodi hiyo ni ya serikali nzima inayojulikana
kama kodi ya ukaguzi zimamoto ambayo hutozwa kwa wafanyabiasha walio na maduka
yanayotambulika kisheria.
Aidha
Kamanda Kakwale akasema kodi hiyo hulipwa
mara moja kwa mwaka mzima na hupelekwa katika mfuko wa serikali kwa
ajili ya majukumu mengine ya kiserikali.
Monday,
14 March 2016
UTEUZI
WAKUU WA MIKOA RUKWA,KATAVI,KIGOMA NA KAGERA WANAJESHI WATUPU(KATIBU TAWALA NA
MKUU WA MKOA KATAVI NI MAJENERALI WA JESHI)
Posted By:Issack Gerald | At:Monday, March
14, 2016
Na.Issack Gerald
Machi
13 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli Machi 13 alifanya
uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 wakiwemo 13 wapya na 13 waliokuwa katika serikali
ya awamu ya nne ya serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais Dk.Jakaya Mrisho
Kikwete.
Katikia Uteuzi huo wamo wanawake watano ambao ni,
Anna
Malecela Kilango
|
Shinyanga
|
Amina
Juma Masenza
|
Iringa
|
Halima
Omary Dendegu
|
Mtwara
|
Dkt.
Rehema Nchimbi
|
Njombe
|
Chiku
Galawa
|
Songwe(Mkoa
mpya)
|
Wakuu
wa Mikoa waliotemwa ni Ludovick Mwananzila (Tabora), Fatuma Mwassa (Geita),
Issa Machibya (Kigoma), Mwantumu Mahiza (Tanga), Parseko Kone (Singida) na
Abbas Kandoro (Mbeya).
Wengine
ni Magalula Saidi Magalula (Rukwa) Rajabu Rutengwe (Morogoro), Dk Ibrahim
Msengi (Katavi), Asery Msangi (Mara), Elaston Mbwilo (Simiyu) na Ali Rufunga
(Shinyanga).
Katika
Uteuzi mpya wa wakuu wa mikoa,umewapa nafasi wanajeshi wanne kuwa wakuu wa
mikoa.
Wanajeshi
walioteuliwa kuwa Wakuu wa Mikoa wapya ni Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga
anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na Meja Jenerali mstaafu, Salum Kijuu
anayekwenda Mkoa wa Kagera.
Majenerali
wengine ni Meja Jenerali mstaafu, Raphael Muhuga anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Katavi na Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga anakuwa Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma.
Uteuzi
wa Majenerali kuwa wakuu wa mikoa ulianza kuzua maswali mengi kwa wananchi
kulikoni ambapo Machi 15 wakati wakuu hao wa mikoa wakila kiapo Mh.Rais alitoa
ufafanuzi huku akitoa wito kwa viongozi hao wa mikoa ikiwa ni sambamba na wakuu
wote wa mikoa kuhakikisha usalama unakuwepo.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli aliwataka wakuu wa Mikoa hao Kuhakikisha wanalinda
Usalama wa Mipaka ya nchi na Kuhakikisha kila Mtanzania anafanya kazi huku
akiagiza Kukamatwa kwa Vijana wanaocheza Michezo ya pulu wakati wa Kazi badala
ya Kufanya kazi.
TUANGAZIE
KATIKA SUALA LA MISHAHARA HEWA
Machi
15 Wakati wakila kiapo cha maadili utii na utumishi wa umma,Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli alitoa siku kumi na tano kwa
Wakurugenzi wa halamshauri zote nchini Kufuta Majina ya Wafanyakazi hewa
wanaolipwa Mishaha.
Katika
nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mkoa wa Katavi sasa utakuwa na wakuu wa Mikoa
watatu tangu kuidhinishwa kwake rasmi mwaka 2012.
1.Dk.Rajabu
Mtumwa Lutengwe
2.Dk.Ibrahim
Hamisi Msengi na
3.Jeneral
Raphael Mugoya Muhuga wa sasa
Mikoa
ya Rukwa,Katavi na Kigoma inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande
wa Magharibi,Rwanda na Burundi Upande wa Kaskazini huku Mkoa wa Kagera
ukipakana na Rwanda Upande wa Magharibi,Burundi upande wa Kusini na Nchi ya
Uganda Upande wa Kaskazini.
Na mara hii tukiangalia matokeo ya Agizo la Mheshimiwa Rais
kuhusu watumishi hewa mpaka Machi 30 siku 15 alizokuwa ametoa zikiwa zimekamilika
huku wakuu wa mikoa 26
ya Tanzania Bara wakiwa tayari wamekabidhi ripoti za uhakiki wa watumishi hewa
katika mikoa yao.
Katika ripoti hiyo inaonesha Mkoa wa Shinyanga kutokuwa na
mtumishi hewa yeyote kati ya watumishi hewa zaidi ya 2000 huku mkoa wa Mwanza ukiongoza
kwa kuwa na watumishi hewa 334.
Watumishi hao zaidi ya 2,000 wameisababishia serikali hasara
zaidi ya Shilingi Bil.4 ,huku baada ya mkoa wa Mwanza kuongoza kwa watumishi
hewa mikoa mingine yenye kiwango cha juu ikiwa ni Singida, Kigoma, Pwani,
Dodoma, Morogoro na Kilimanjaro.
Ripoti hizo ziliwasilishwa jijini Dar es Salaam jana na Wakuu
wa Mikoa hao kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene.
KATIKA MKOA WA KATAVI
Watumishi
hewa waliobainika wako 21 ambapo serikali ya Tanzania katika mkoa wa Katavi
Pekee imepata hasara ya Milioni 20.7.
Wednesday,
16 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, March
16, 2016
Wasichana
wapatao 500 wanaodaiwa kufanya biashara ya ukahaba nchini Tanzania pamoja na
wateja wao zaidi ya 200 wanashikiliwa na polisi nchini.
Walikamatwa
kufuatia msako unaoendelea kukomesha biashara hiyo ambayo haikubaliki kwa
mujibu wa sheria nchini humo.
Hii
ni idadi kubwa kuwahi kukamatwa katika vita dhidi ya biashara ya ukahaba nchini
humo.
Wengi
walikamatwa maeneo ya Kinondoni, Temeke na Ilala 51.
Kamishna
wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema wengi wa
majambazi hukimbilia kwa biashara ya ukahaba.
“Kuwakamata
na kuwahoji kunasaidia kupata mambo mengi sana kuhusiana na haya (uhalifu),
hata madawa ya kulevya pia. Wengi unakuta wanajua watu wanaoyatumia, wengine
wanashiriki,” aliambia wanahabari.
Aliwaomba
wananchi kuwasiadia maafisa wa polisi katika operesheni hiyo.
Thursday, 17 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, March
17, 2016
Na.Issack Gerald-Katavi
Oparesheni
za kuwataka wanaomiliki silaha kuzihakiki linaendelea ambapo Machi 17 mwaka
huu,Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi liliwataka wananchi wanaomiliki silaha
kinyume cha sheria kuzisalimisha mara moja silaha hizo katika vituo vya Polisi
vilivyopo karibu na makazi yao.
Agizo
hilo lilitolewa na Kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed akisema
kuwa jeshi la polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu au
kikundi kitakachobainika kumiliki silaha kinyume cha sheria na taratibu za
nchi.
Aidha,
Kamanda alisema walio na silaha majumbani mwao ambazo zilikuwa zikimilikiwa
kihalali na kwa sasa ndugu zao waliokuwa wakimiliki silaha hizo na walikwishafariki
dunia wafuate utaratibu kwa kuzisalimisha silaha hizo ambapo suala hili
linawahusu pia wazee ambao wamefikisha umri usiowaruhusu kumiliki silaha.
Hata
hivyo alisema kuwa ni kosa kisheria wanaomiliki silaha kisheria kuziazimishwa
kwa makampuni bina binafisi ya ulinzi ambapo pia aliwataka kuacha tabia hiyo
mara moja.
Kamanda
Mohamed alisema wananchi wanatakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la
polisi wanapoona viashiria vyovyote vya uharifu ili vidhibitiwe kabla ya kuleta
madhara.
WAKAZI
WAISHIO MLIMA WA LIAMBA LYAMFIPA WATAKIWA KUHAMA KABLA NGUVU YA JESHI KUTUMIKA.
Na.Issack Gerald-Mlele
Machi
22,baadhi ya wakazi waliojenga nyumba na kuanza kufanya shughuli mbalimbali
ikiwemo kilimo katika mlima wa Liamba Lyamfipa uliopo Wilayani Mlele Mkoani
Katavi walipewa wito wa kuhama mara moja sehemu hiyo.
Ujumbe
huo uliotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw.Issa Suleiman Njiku Kupitia kilele
cha maadhimisho ya siku ya wiki ya maji yalifofikia kilele chake Machi 22 mwaka
huu maadhimisho hayo yakifanyika katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe,ambapo watendaji
wa vijiji,kata na wenyeviti wa vijiji waliamriwa kusimamia zoezi la kuwaondoa
wakazi hao.
Aidha
Njiku aliwataka wananchi kuwa waangarifu katika mlima huo na kutafakari madhara
yatakayojitokeza ikiwa mlima huo watauharibu.
Alisema
wakazi watakaokaidi kuondoka katika mlima wa liamba Lyamfipa watafuatwa na mkuu
wa Wilaya akiwa na Askari ili kuwatoa
kwa nguvu.
Awali
katika ufunguzi wa maazimisho ya wiki ya maji duniani,serikali ya Mkoa wa
Katavi ilisema kuwa itaendelea kulinda vyanzo vya maji vilivyopo Mkoani Katavi
ikiwa ni sambamba na kutafuta namna ya kuendelea kutatua changamoto za baadhi
ya wananchi hususani kukosa maji.
Hata
hivyo baadhi ya wakazi katika Manispaa ya Mpanda walisema kuwa hawaoni haja ya
kuwa na maadhimisho ya wiki ya maji ikiwa mwananchi anaendelea kukosa maji ya
kunywa yaliyo safi na salama.
Maadhimisho
ya Wiki ya maji duniani huanza kila mwka machi 16 ha kufikia kilele chake machi
22.
HATIMA YAKE
Mpaka
naingia katika mitambo ya Mpanda Radio fm taarifa iliyopo ni kuwa wakazi hao wameondoka
katika eneo hilo hususani katika vyanzo vya maji Kasansa huku baadhi ya wakazi
wakielezwa kutoka Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa hii ikiwa imethibitishwa baada ya
Kanali Issa Suleimani Njiku kufanya ziara.
C.W.T
YAWAMWAGIA MABATI WALIMU WASTAAFU MKOANI KATAVI
Na.Issack
Gerald-Mpanda
CHAMA
cha walimu C.W.T Mkoani Katavi kimekabidhi mabati 20 kwa walimu 11 wastaafu
kutoka katika halamshauri za Nsimbo na Mpanda kwa kila mmoja kama sehemu ya
kutambua mchango wao katika sekta ya elimu.
Akikabidhi
mabati hayo Machi 24,2016,mjumbe wa kamati ya C.W.T taifa Bw.Costantine Marisel
aliwataka walimu kuendelea kuzingatia maadili ya kazi yao.
Alisemakuwa
miongoni mwa tabia zinazotakiwa kuepukika ni pamoja na walimu wa kiume
kutofanya mapenzi na watoto wa kike,walimu wa kike kufanya mapenzi na wanafunzi
wa kike na walimu kuwachangisha fedha wanafunzi fedha ambazo hazitakiwi
kuchangwa kwa kuwa kuna sera ya elimu bure.
Pamoja
na mambo mengine,nao baadhi ya walimu waliopata msaada huo walikishukuru chama
cha walimu CWT kwa kuwajali huku wakisema kuwa ni vizuri kuzingatia pia usafiri
wao kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kutekeleza majukumu
yao.
Hatua
hiyo CWT pia ilipongezwa na wadau
mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi wakisema kuwa hata taasisi nyingine zenye
uwezo zifanye hivyo kwa ajili ya kuwasaidia kwa kuwa walitoa mchango mkubwa
katika utumishi wao.
WAHITIMU MAFUNZO YA
UHIFADHI HIFADHI ZA TAIFA WILAYANI KATAVI
Na.Agness Mnubi-Mlele
Machi
24,wahitimu wa Mafunzo ya Kujengwa uwezo wa uongozi katika uhifadhi wa hifadhi
za taifa nchini walitakiwa Kujenga Mahusiano Mazuri na Jamii zinazozunguka
hifadhi ili kuwawezesha kupata taarifa
za watu wanaojihusisha na matukio ya ujangili.
Kauli
hiyo imetolewa na Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Katavi Luteni Kanali Alex Ntazi Wakati wa hafla ya Kufunga Mafunzo hayo iliyofanyika
Katika Kituo cha Mafunzo Kilichopo Wilayani Mlele Mkoani hapa.
Bw.Ntazi aliwataka wahitimu kuepuka vitendo
vya rushwa,matumizi mabaya ya silaha,ulevi na utovu wa nidhamu na badala yake
walinde rasilimali za taifa.
Aidha
alisema wanatakiwa kuwa na mahusiano na watu wanaozunguka maeneo ya hifadhi ili
kupatiwa taarifa sahihi za ujangili unaofanywa na waharibifu wa rasilimali za
nchi.
Kwa
upande wake kaimu mkurugenzi mkuu wa hifadhi za taifa Tanzania Bw.Ntango Mtaiko
aliwataka wahitimu kuzingatia nidhamu ya kazi na kupamana na ujangili na
kudumisha ushirikiano kati yao wenyewe na ndipo wahushe wengine.
Naye
Mkurugenzi utumishi na utawala hifadhi za taifa tanapa Bi.Witness Shoo aliwataka
wahitimu kufauata sheria,kanuni,taratibu na maelekezo katika kutekeleza
majukumu.
Awali
akisoma taarifa ya kituo cha hifadhi cha mlele kaimu meneja mapori ya akiba
Rukwa na Huhafwe Mark Chuwa aliiomba idara ya wanyama pori hifadhi za taiafa na
Mkoa wa kuujumla kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho ikiwa ni pamoja
na ufinuyu wa bajeti,upungufu wa vitendea kazi,mawasiliano na miundombinu.
Katika
risala ya wahitumu iliyosomwa na mmoja
wa wahitimu Bi Angela Nyaki waliahidi kufanya kazi kwa weledi kwa kutumia
mafunzo waliyoyapata.
Mafunzo
hayo ya wahifadhi yaliyohitimishwa Machi 23,yaligawanyika katika makundi mawili
amabpo kundi moja lilianza Februari 01 mwaka huu na kumalizika Februari 16
mwaka huu huku kundi la pili likianza Februari 22 na kuamlizika Machi 23 mwaka
huu.
400 WABAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA
KIFUAKIKUU KATAVI,IMANI ZA USHIRIKINA BADO KIKWAZO.
Na.Issack Gerald-Nsimbo
Machi
24 kila mwaka ni maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kifuakikuu duniani.Kupitia
siku hiyo imegundulika kuwa Zaidi ya
wagonjwa 400 wamegundulika kuwa na maambukizi wa ugonjwa kipindupindu huku
wagonjwa hao wakipatiwa matibabu na habari njema ikiwa ni kuwa hakuna mtu
aliyefariki kutokona na ugonjwa huo.
Takwimu
hiyo iliotolewa na mratibu wa kifuakikuu na ukoma Wilayani Nsimbo Mkoani Katavi
Dk.Gabriel Kalumuna kwa niaba ya Daktari wa kikufua kikuu Mkoa wa Katavi ambapo
amesema kuwa kati ya idadi ya wagonjwa hao hakuna kifo kichojitokeza na wote
walipatiwa matibabu.
Alisema
kuwa baadhi ya watu kuendelea kuwa na imani za kishirikina zinachangia
kuendelea kuwepo kwa ugonjwa huo kwani watu huchelewa kupatiwa matibabu ambayo
hata hakuna malipo yoyote.
Alisema
kuwa vituo vinavyotoa huduma ya kupima kifuakikuu katika Wilaya ya Mpanda ni
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda,Kituo cha Afya Karema,Mwese na Mishamo huku vituo
vyote vya afya vikitoa dawa kwa wagonjwa.
Miongoni
mwa vituo visivyokuwa na uwezo wa kupima ni pamoja na Ilunde.
Aidha
alisema kuwa idadi ya wagonjwa ni wanazidi idadi ya vituo vya afya ambapo
aliiomba serikali kuviwezesha vituo vilivyoko mbali view na uwezo wa kupima
wagonjwa hususani vijijini ambapo vijiji vingi vipo Halmshauri za Wilaya ya
Mlele ,Mpanda Vijiji,Mpimbwe na Nsimbo.
Pamoja
na mambo mengine pia alisema kuwa ugonjwa huu husababishwa na aina ya vimelea vijulikanavyo
kama MICROBACTERIA CHUBA ambapo huenea
kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwenda kwa mtu mwingine asiye na maambukizi
kupitia hewa.
Kuna
aina mbili za kifuakikuu cha mapafu ambazo hushambulia vioungo kama
mifupa,figo,moyo na viungo vingine mwilini ambapo kwa habari nzuri ugonjwa huu
hutibika ikiwa mgonjwa atawahi mapema kuanza matibabu.
Dalili
za ugonjwa huu ni kukohoa kuanzia mwezi mmoja na kuendelea,kukosa hamu ya
chakula,homa za mara kwa mara makohozi yaliyochanganyika na damu,kupungua uzito
na kuhisi kifua kubanwa.
Njia
moja wapo ya kupambana na ugonjwa huu ni kujenga nyumba ambayo ina madirisha
yanayopitisha hewa ya kutosha na kuwahi mapema katika vituo vya afya kupatiwa
matibabu.
Kwa
takwimu ya Wizara ya Afya,watu wapatao 12000 hapa Tanzania hufariki dunia
kutokana na ugonjwa huu.
HABARI
KUHUSU MTO KOGA UNAOTENGANISHA MKOA WA KATAVI NA TABORA
Kufuatia Stendi kuu ya Mabasi
Manispaa ya Mpanda kuwa gizani kwa muda mrefu licha taa kuwepo bila mafanikio
ya kuwaka ilihali uongozi wa Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya kufika mara kadhaa
katika stendi hiyo bila ufumbuzi,Machi 28 Uongozi wa Stendi kuu ya mabasi
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,ulipaza sauti umemwomba Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Meja Jeneral Raphael Muhuga kuingilia kati kutatua changamoto ya kutowaka kwa
taa za umeme katika stendi tangu mwaka jana pamoja na wasafiri kukosa mahali pa
kujikinga mvua na jua.
Ombi hilo likiwa limetolewa na
Mwenyekiti Msaidizi wa Stend Bw. Ramadhani Salm Nkwizu wakati akizungumza na
Mpanda Radio Katika stendi hiyo akisema kuwa licha ya Mkurugenzi wa Manispaa ya
Mpanda na Mkuu wa Wilaya Mpanda kuahidi kutatua changamoto hiyo tangu mwaka
jana,hakuna kilichotekelezeka mpaka sasa.
Kwa upande wake Jailos Kipenye
amesema kuwa watu wamehofia kuingiliwa na waharifu pamoja na kuibiwa mali zao
kutokana na kutokuwepo kwa mwanga nyakati za usiku.
Suala la barabara kutoka Mpanda
Kupitia Tabora ikiwa ni takribani miezi 3 sasa tangu katazo la kutumia barabara
hiyo kutumika kutolewa wasafirishaji na wasafiri wanakumbwa na adha ya kutofika
Tabora kwa muda mwafaka pamoja na
wasafiri kutumia kiasi kikubwa cha nauli.
Aidha viongozi hao wakamwomba mkuu wa
Mkoa kushughulikia tatizo la barabara inayoanzia Mpanda hadi Tabora.
Kufuatia hali ya sintofahamu juu ya
hatima ya barabara kutoka Mpanda Kuelekea Inyonga hadi Tabora,Machi 25 mwaka
huu,Mkuu wa Mkoa wa Katavi alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara
kutoka Mpanda Kuelekea Tabora aliitaka serikali ya Wilaya ya Mlele kuendelea
kuzuia magari makubwa yakiwemo ya abiria kutoruhusiwa kupita katika barabara
hiyo kwa kuwa msimu wa mvua za masika unaendelea isipokuwa akasema kuwa magari
madogo yasiyo ya abiria yanaruhusiwa kupita.
Mto Koga hupokea maji kutoka mito ya
Rungwa na Chunya kupitia ziwa Rukwa
Barabara ya kutoka Mpanda Katavi hadi
Tabora ilizuiliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Msengi
aliyezuia barabara hiyo kutumiwa na vyombo vya usafiri Januari 26 mwaka
2016,kutokana na daraja la mto Koga linalotenganisha Mkoa wa Katavi na Tabora
kukatika ambapo jumla ya watu 10 walikufa maji baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kusombwa na maji.
TUZO
KWA H(W) MPANDA
MPANDA.
Aggy
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Mpanda imepokea cheti na fedha kiasi cha shilingi Million mia mbili kumi na nne mia tatu
arobaini na sita elfu kutoka Wizara ya
elimu ,sayansi na mafunzo ya ufundi kwa kukidhi vigezo vya
matokeo ya utendaji kazi wa kila siku.
Akizungumza
na Mpanda redio Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpanda ambaye pia ni Afisa
Elimu idara ya Msingi Kennedy Shilumba amevitaja vigezo vilivyozingatiwa katika utoaji wa
zawadi hiyo ikiwa ni pamoja na huduma bora kwa walimu,na utendaji mzuri wa
kazi.
Amefafanua
kuwa wamesubiri kupewa maelekezo ya matumizi ya fedha hizo kutoka Wizara lakini
wamedhamilia kuzitumia katika kutatua miundo mbinu na madawati katika shule za
msingi na sekondari.
Halmashauri
ya Mpanda imekuwa ya tisa kati ya Halmashauri 10 bora zilizopata zawadi hiyo Kitaifa.
C.W.T
KATAVI WAFANYA MAANDAMANO KUDAI MALIMBIKIZO YA MADAI YAO
Na.Issack Gerald-Katavi
MACHI 31,CHAMA cha walimu C.W.T Mkoani
Katavi kimefanya maandamano ya amani kushinikiza kulipwa madai ya mishahara yaliyodumu
takribani miaka mitatu bila kupatiwa ufumbuzi.
Akizungumza wakati wa maandamano hayo
mbelel ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,mwenyekiti wa wa Chama cha walimu
Wilaya ya Mpanda Mwalimu Jumanne Msomba amesema wanachohitaji ni majibu kutoka
kwa mwajiri wao namna watakavyolipwa madai yao.
Akizungumza na walimu hao nje ya
Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda,Katibu wa CWT Wilison Msolwa amesema
sababu kubwa ambayo imewapelekea waandamane ni kikwazo cha muda mrefu
kuhusoiana na madai yao.
Walimu hao wanaokaribia 80 wanaotoka
katika shule mbalimbali zilizopo Wilayani Mpanda wameshiriki maandamano hayo.
Hata hivyo mapema asubuhi ya machi 31
mwandishi wetu aliyekuwepo wakati wakiandamana ameripoti kuwa kwa mjibu wa
walimu hao wanaounda chama cah C.W.T walisema kila ofisi waliyokuwa wakiingia
kupata majibu ya madai waliambiwa hakuna msemaji.
Endelea kufuatilia
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kwa habari za ndani na nje ya Katavi.
Kwa maoni p5tanzania@gmail.com
Comments