HALMSHAURI YA WILAYA YA MPANDA WAIBUKA NA TUZO YA CHETI KILICHOAMBATANA NA MIL.214,346,000/=
Na.Issack Gerald-Katavi
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Mpanda imepokea cheti na fedha kiasi cha shilingi Million mia mbili kumi na nne mia tatu
arobaini na sita elfu kutoka Wizara ya
elimu ,sayansi na mafunzo ya ufundi kwa kukidhi vigezo vya matokeo ya utendaji kazi wa kila siku.
Akitolea
ufafanuzi kuhusu tuzo hiyo,Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda
ambaye pia ni Afisa Elimu idara ya Msingi Kennedy Shilumba amevitaja vigezo vilivyozingatiwa katika utoaji wa
zawadi hiyo ikiwa ni pamoja na huduma bora kwa walimu,na utendaji mzuri wa
kazi.
Amefafanua
kuwa wamesubiri kupewa maelekezo ya matumizi ya fedha hizo kutoka Wizara lakini
wamedhamilia kuzitumia katika kutatua miundo mbinu na madawati katika shule za
msingi na sekondari.
Halmashauri
ya Mpanda imekuwa ya tisa kati ya Halmashauri 10 bora zilizopata zawadi hiyo Kitaifa.
Comments