MGOGORO WA ENEO LA UCHIMBAJI MADINI MTAA WAELEKEA PAZURI
Na.Issack Gerald-Mpanda
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza
Mwamlima amesema mgogoro wa ardhi katika eneo la machimbo ya kokoto na madini
aina ya dhahabu uliopo katika kijiji cha Kampuni unatafutiwa ufumbuzi.
Amesema hayo machi 31,2016 alipokuwa
akijibu hoja kuhusu hatima ya malalamiko ya wakazi wa eneo hilo kuilalamikia
serikali kwa madai ya maeneo hayo kuchukuliwa na jeshi.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa ,serikali
inafanya jitihada kuhakikisha inamaliza migogoro baina yake na wananchi ili
kujenga uwajibikaji wa dhati katika shughuli za maendeleo.
Sanjari na hayo Mwamlima amewataka
askari wa wawanyamapori katika hifadhi ya taifa Katavi pamoja na jopo zima la
uongozi ndani ya hifadhi hiyo kujichunguza kwanza wao wenyewe kwanza kabla ya
kutekeleza adhima ya serikali katika mapambano dhidi ya Ujangiri.
Eneo hilo la wachimbaji lina
wachimbaji zaidi ya 200 walioanza kuchimba dhahabu tangu mwaka 1980 ambapo zuio
la kutochimba dhahabu katika mlima wa kampuni lilitolewa mapema mwezi Januari
mwaka huu na Ofisi ya madini na jeshi.
Comments