C.W.T KATAVI WAANDAMANA KWA MKURUGENZI MANISPAA KUDAI ZAIDI YA MILIONI 100 WANAZODAI KWA MIAKA 3 BILA MAJIBU
Na.Issack Gerald-Mpanda
CHAMA
cha walimu mkoa wa katavi (CWT) kimefanya maandamano katika ofisi za mkurugenzi wa manispaa ya
mpanda kwa lengo la kushinikiza kulipwa madai yao.
Akizungumza
kwa niaba ya wanachanma hao mwenyekiti
wa CWT Mkoa wa Katavi Bw Gregory Mshota alisema
madai hayo ni sugu na yamedumu muda mrefu hivyo wanahitaji ufumbuzi wa
haraka.
Amesema
jumla ya deni wanalo dai ni ya zaidi ya
shilingi milioni mia moja ambazo
wamekuwa wakifuatilia kwa muda mrefu bila kuwa na majibu ya kulidhisha .
Kwa
upande wa Katibu wa CWT Wilison Msolwa alisema sababu kubwa ambayo imewapelekea
waandamane ni kikwazo cha muda mrefu kuhusoiana na madai yao.
Walimu
ambao ni wanachama wa CWT wapatao 80 wanaotoka katika shule mbalimbali zilizopo
Wilayani Mpanda wameshiriki maandamano hayo.
Kwa
upande waken kaimu mkurugenzi wa manispaa ya mpanda Bi. Enelia Lutungulu mekiri
kuwepo kwa tatizo hilo na kuwaahidi wanachama hao kushughulikia madai yao ndani ya miezi miwili
kuanzia Machi 31.
Comments