WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUTOFANYA KAZI KWA NIDHAMU YA WOGA,MABILIONI YAOMBWA KUIDHINISHWA KUFANIKISHA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MPANDA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Watumishi wa umma Wilayani Mpanda
Mkoani Katavi,wametakiwa kutofanya kazi kwa nidhamu ya woga na badala yake
watumie taaaluma waliyoisomea.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw.Pazza Mwamlima(PICHA NA.Issack Gerald) |
Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima kikao cha kamati ya ushauri ambacho kimefanyika
kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kikao ambacho
kimefanyika jana katika ukumbi wa iadara ya maji Mjini Mpanda.
Katika hatua nyingine,Mkurugenzi wa
Idara ya maji Mkoani Katavi Injinia Zacharia Nyanda amesema chanzo kikuu
kinachosababisha maji kutopatikana kwa maji katika baadhi ya maeneo ya manispaa
ya Mpanda ni uzarishaji mdogo wa maji.
Kikao hicho ambacho kimefanyika ukmbi
wa idara ya maji kinawahusisha viongozi na wakuu wa idara mbalimbali wakiwemo
Wakurugenzi ngazi ya Wilaya na Mkoa.
Akiwasilisha taarifa katika kikoa
hicho cha kupitisha mpangao wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/2017,Mchumi wa Manispaa
ya Mpanda Bi.Mary Kanumba,katika taarifa yake ameiomba serikali kuidhinisha bajeti
ya shilingi bilioni 23.8. kwa ajili ya kuekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
na shughuli nyingine za kiutawala na maendeleo.
Amesema kuwa,Shilingi Bil.19.3 ni kwa
ajili kwa bajeti ya kawaida na Shilingi Bil.4.4 nje ya komo wa bajeti.
Bi.Kanumba Mapato ya ndani katika
Manispaa,amesema kuwa pato limeongezeka kutoka Shilingi Bil.1.9 hadi Shilingi Bil.2.3
ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 18.5 ambapo ongezeko hilo limechangiwa
na vyanzo mbalimbali vya mapato vikiwemo kodi ya majengo,ushuru wa zao la tumbaku,leseni
za biashara,minada na ushuru wa vileo.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mpanda katika mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017,katika taarifa
ambayo imesomwa na Mchumi wa Halmshauri ya hiyo Bw.Filemon Mrageri,Halmshauri ya
Mpanda imeomba kuidhinishiwa Shilingi Bilioni Bil 31 Mil.584 laki moja
thelathini na sita elfu mia saba na arobaini (31,584,136,740) kwa ajili ya
kutekeleza miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.
Hata hivyo,bajeti ya malipo ya
mishahara ya wafanyakazi imeonekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa miongoni mwa
sababu ikiwa ni utanuzi wa mipaka ya utawala na ajira mpya kwa watumishi katika
Halmashauri zote za Manispaa ya Wilaya ya Mpanda.
Kikao hicho muhimu katika Halimashauri,kimeshirikisha
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima ambaye ndiye mwenyekiti wa
kikao,wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya ya
Mpanda,wakuu wa idara mbalimbali katika katika halimshauri zote,watendaji wa
kata na baadhi ya viongozi kutoka Idara katika ngazi ya Mkoa akiwemo Meneja wa
Idara ya Maji Mpanda Injinia Zacharia Nyanda na Meneja Mpya wa wa Kwanza wa
Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Katavi.
Comments