MKURUGENZI IDARA YA MAJI KATAVI ATOA MATUMAINI KWA WAKAZI WA MPANDA,MGAO WA MAJI KUWA HISTORIA


Na.Issack Gerald-Katavi
Idara ya Maji Mkoani Katavi imesema kuwa mradi wa Orestria unaoshughulikia ukarababti na ujenzi wa mambomba na vyanzo vya maji unaotarajia kuanza mwezi ujao,kutawaondolea wananchi adha ya kukosekana kwa maji na hivyo maji kupatikana kwa saa 24 katika mji wa Mpanda.
                                          
Mradi wa maji wa Ikorongo wenye lita 1,000,000 moja ya chanzo cha maji kinachosambaza maji Mkoani Katavi (PICHA NA Issack Gerald)

Baadhi ya Wananchi wakiwa wametembelea mradi wa maji wa Ikorongo (PICHA NA Issack Gerald)



Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Maji Mkoa wa Katavi Injinia Zzacharia Nyanda wakati akijibu hoja za wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri cha kupitisha mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa idara ya maji.
Amesema kuwa mradi huo pamoja na kuweka mabomba mapya ya kupitisha maji,mradi huo unataraji kujenga chanzo cha Maji Ikorongo Na.2 ili kupata tenki lenye ujazo wa lita milioni moja huku tenki linguine likjengwa vijijini.
Hata hivyo Injinia Nyanda amesema kuwa ikiwa mradi wa Oretria hautakuwepo,Shilingi milioni 7 zitahitajika ili kuondoa  kabisa tatizo la mgao wa maji katika Manispaa ya Mpanda.
Aidha amesema kuwa tatizo linguine linalopelekea maji kukosekana kwa kiwango kikubwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi hususani Manispaa ya Mpanda ni kunatokana na kiasi kidogo cha uzalishaji wa maji katika Manispaa ya Mpanda,mabomba yenye upana mdogo tena ya chuma,mabomba kuziba na mengine kukatika kutokana na mabomba hayo kuwa ya muda mrefu.
Amesema kuwa kiwango cha maji kinachozalishwa ni lita mil.3,360,000 huku mahitaji yakiwa ni lita mil.9,500,000 ambapo kwa kiwango hicho ni sawa na upungufu wa lita mil.6,140,000.
Baadhi ya mitaa ya kilimahewa,Kawajense ,Rungwe,Nsemulwa migazini,Aitel na Ilembo hazina matatizo makubwa ya ukosefu wa maji huku Kata ya Makanyagio na Mpanda Hotel zikiongoza kwa kuwa na mabomba yaliyoziba mabomba yenye upana mdogo na kukumbwa na mgao wa maji mara kwa mara..

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA