MKURUGENZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO ATAKA WANAFUNZI WASOME MASOMO YA SAYANSI
Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
WANAFUNZI
wa Shule za Sekondari katika Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani katavi
wametakiwa kusoma masomo ya sayansi.
Wito
huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Michael Nzyungu wakati
akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA
sambamba na Mpanda redio,akisema kuwa wanafunzi wajitokeze kwa wingi kusoma
masomo ya sayansi ili kufaidi maabara zilizopo katika shule za sekondari za
Halmashauri ya Nsimbo.
Amesema
Lengo la Serikali kujenga maabara kila shule ya sekondari ni kuinua kiwango cha
elimu kwa masomo ya sayansi hivyo wanafunzi hawana budi kusoma masomo ya
sayansi ili kutumia maabara hizo.
Amesema
wanazidi kuboresha maabara hizo kwa kuhakikisha kuwa na miundombinu mizuri, kuongeza vifaa vya kutosha na walimu wa masomo ya
sayansi.
Kauli
ya mkurugenzi mtendaji huyo inakuja ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha
wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa lengo la kupata wataalamu katika masuala
mbalimbali hapa nchini.
Hata
hivyo licha ya hamasa hiyo,kunahitajika walimu zaidi wa masomo ya sayansi wenye
uwezo thabiti.
Comments