MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MKOA WA KATAVI AFIKISHWA MAHAKAMANI AKITUHUMIWA KUMTOROSHA ALIYETAKA KUMUUA KWA KUKATA KIGANJA CHA MKONO MLEMAVU WA NGOZI ALBINO,WAMO PIA ASKARI MAGEREZA WAWILI WILAYANI MPANDA NA WALIOKUWA WAKITOROSHWA WADAKWA TENA.
Na.Issack
Gerald-Katavi
Watu watano akiwemo
Mwanasheria Mkuu Mkoani Katavi Bw. Falhati Seif
Khatibu (45),wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma
za kumtorosha mtuhumiwa Alex Manyanza
Enock (27) Mkazi wa majimoto aliyekuwa anakabiliwa na kesi NA. MTO/IR/76/2015 ya
kujaribu kuua mlemavu wa Ngozi Albino Limi Luchoma(30) mkazi wa kijiji cha
Mawiti kata ya Majimoto Wilayani Mlele.
Kaimu kamanda wa Polisi
Mkoani Katavi Rashid Mohamed,amewataja watuhumiwa kwa ujumla kuwa ni A. 287 Sajenti
John Musa (50) mkazi wa mtaa wa mji mwema Wilayani Mpanda, A. 5385 Sajenti
Deogartius Katani (50) Mkazi wa mtaa wa Kigamboni Wilaya ya Mpanda wa gereza la
mahabusu Mpanda.
Kamanda pia amewataja
wengine wanaotuhumiwa kuwa ni Mwanasheria mkuu wa Mkoa wa Katavi Falhati Seif
Khatibu (45) mkazi wa maeneo ya Msakila Shule ya Msingi ,Masanja Kasinje
Kasala(33) mkazi wa Kakese Mkwajuni Wilayani Mpanda pamoja na Ngassa Mashindike
(37) mkazi wa Majimoto Wiayani Mlele.
Kamanda Mohamed amesema kuwa mnamo 19.01.2016 majira ya
saa 09:30 asubuhi,Jeshi la Polisi Mkoani Katavi lilipokea taarifa toka kwa raia
wema kuwa mtuhumiwa Alex Manyanza Enock hayupo
gereza la mahabusu Mpanda.
Baada ya taarifa hizo
kupokelewa,jeshi la polisi lilianza upelelezi na kubaini kuwa mtuhumiwa huyo
alitoroka tangu tarehe 12.10.2015 katika gereza la mahabusu Mpanda ambapo awali
mtuhumiwa huyo aliwahi kutoroka akitumikia kifungo cha miaka 5 kwa kosa la wizi
wa mifugo katika gereza la kilimo la Kalilankulukulu kabla ya kukamatwa kwa
kesi hii ya kujaribu kuua.
Kamanda ameendelea
kufafanua kuwa,ilipofika 21.01.2016 wakati jeshi la polisi likiendelea na
upelelezi wa kesi hiyo,zilipokelewa taarifa za kuwa mtuhumiwa Alex Manyanza
Enock anapatikana Mkoani Rukwa ambapobaada ya ufuatiliaji,mtuhumiwa alipatikana
akiwa amejificha katika kijiji cha Kipande Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.
Katika mahojiano ya kina,mtuhumiwa
Bw. Alex Manyanza Enock alieleza jinsi alivyofanikishiwa mipango ya kutoroka
gerezani akimtaja mjomba wake Bw.Masanja Kasinje Kasala pamoja na rafiki yake
Ngassa Mashindike ambao naobaada ya kukamatwa walikiri kufanya mipango ya
kumtorosha mtuhumiwa kwa lengo la kuwafanya watuhumiwa wengine katika kesi yao
ya kujaribu kuua kutotiwa hatianki akiwemo mjomba wake walioko pamoja katika
kesi hiyo Bw.Masunga Kashinje.
Mtuhumiwa alieleza kuwa
waliwashirikisha askari magereza wawili ambao ni A. 287 Sajenti John Musa
Masagula na A. 5385 Sajenti Deogratius
Katani wote wakazi wa kituo cha kazi gereza la mahabusu Mpanda ambao walipatiwa
kiasi cha Shilingi milioni moja(1,000,000/= ) ili kumwezesha
mtuhumiwa kutoroka.
Pia walimtaja mwanasheria
mkuu wa serikali ya Mkoa wa Katavi Bw. Falhati Seif Khatibu ambapo walidai walimpatia kiasi cha shilingi
milioni mbili (2,000,000/=)ili kumwondolea shitaka mtumiwa Masunga Kashinje baada
ya kuwa mtuhumiwa Alex Manyanza Enock amefanikiwa kutoroka.
Hata hivyo,Kamanda wa
polisi Mkoani Katavi ametoa wito kwa watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi
kufanya kazi kwa kufuata misingi ya utumishi huku wakiendelea kuihudumia jamii
kwa ukaribu.
Mshirikishe na mwenzako
Comments