KAMANDA WA POLISI MWANZA ATOA TAARIFA YA ASKARI KUMUUA KWA RISASI ASKARI MWENZAKE
NA.Mwandisi
wetu-MWANZA
Askari
mmoja wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza jana amefyatua risasi na
kumuua asikari mwenzake kisha nayeye kujipiga risasi na kufariki dunia katika
lindo la benki ya posita jijini mwanza huku chanzo cha tukio hilo kikiwa hakija
julikana.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi wa Polisi Justus Kamugisha
amethibitisha kutokea kwa tukio na kwamba limetokea majira ya saa nane na nusu
mchana katika lindo la Banki ya Posta tawi la Pamba jijini Mwanza.
Kamanda
Kamugisha amewataja askari hao kuwa ni Konstebo H 852 Daud Masunga Elisha
aliyempiga risasi Pc Petro Simoni Matiko H5950 eneo la begani na baadae Pc
Masunga kujipiga risasi eneo la paji la uso na kufariki pao hapo, wote ni
askari wa wilaya ya Nyamagana
Aidha
Kamanda Kamgisha amesema jeshi la Polisi lina endelea na uchunguzi juu ya tukio
hilo ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.
Comments