BODABODA MPANDA WAZUNGUMZIA MIUNDOMBINU MIBOVU YA BARABARA INAVYOATHIRI UCHUMI WAO
Na.Issack
Gerald-MPANDA
Miundombinu mibovu ya barabara hususani
kipindi hiki cha masika imeathiri uchumi wa waendesha pikipiki katika Manispaa
ya Mpanda Mkoani Matavi.
Hayo yamebainishwa na waendesha
pikipiki hao wakati wakizungumza na P5
TANZANIA MEDIA na mpanda redio ambapo wamesema kuwa barabara nyingi hasa
vijijini hazipitiki kutokana na mabonde hali inayowafanya kufanya shughuli
hiyo mjini pekee.
Katika hatua nyingine madereva hao
wamesema,katika kuzua ajali za barabarani hasa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu
wamejipanga kuendesha pikipiki kwa umakini mkubwa kutokana ongezeko la vyombo vingi
vya moto barabarani.
Takwimu zinaonyesha kuwa katika
kipindi cha sikukuu matukio ya ajali huongezeka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo
madereva kuendesha kwa mwendokasi pamoja na ulevi.
Comments