AKIMBIA MKONO WA POLISI KUKWEPA KUKAMATWA KWA KOSA LA KUMILIKI SILAHA KINYUME NA SHERIA
Na.Issack
Gerald-Mpanda
Jeshi la polisi Mkoani Katavi linamtafuta mtu mmoja
aliyekimbia akikwepa kukamatwa na polisi kutokana na kumiliki silaha aina ya gobore kinyume na sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari amethibitisha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Malugumba Nzinza kukamatwa
na silaha aina ya gobore ambayo imepatikana ikiwa imefichwa katika nyumba yake.
Kamanda
kidavashari amesema mtu huyo alikamatwa,mnamo tarehe 12.12.2015 majira ya saa
12:00 katika kijiji cha Mpembe Kata na
Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda Mkoa wa
Katavi.
Kamanda amesema kuwa katika tukio hilo,Jeshi
la Polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori (TANAPA) walipata taarifa
toka kwa raia wema kuwepo kwa mtu anayehisiwa kumiliki silaha kinyume na
utaratibu.
Mpaka sasa mtuhumiwa bado hajakamatwa na
misako mbalimbali inaendelea katika kuhakikisha mtuhumiwa anatiwa nguvuni na
kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Comments