Posts

MWANAMKE ASIYEJULIKANA ATUPA MTOTO WA UMRI WA SIKU 1 KATIKA UWANJA MICHEZO

Mtoto wa jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa na umri wa   siku 1 ameokotwa akiwa hai katika uwanja wa Azimio   Halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi baada ya kutupwa   na mwanamke ambaye mpaka sasa hajafahamika majina wala makazi yake. Mashuhuda wa tukio wakilaani tukio hilo,wamesema mtoto huyo inasadikiwa alitupwa Ijumaa ya Juni 8 mwaka huu majira ya mchana mpaka alipookotwa majira ya saa kumi   jioni . Hata hivyo wananchi wilayani Mpanda wamesikitishwa na tukio hilo na kuomba   hatua kali zichukuliwe dhidi ya mwanamke atakayebainika kutenda unyama huo dhidi ya mtoto asiyekuwa na hatia. Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii manispaa Redgunda Mayorwa amethibitisha kupokea taarifa za mtoto huyo ambapo amesema jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kumpata na kumfikisha katika vyombo vya sheria mwanamke aliyetenda unyama huo. Aidha ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali na jeshi la Polisi kuhusiana n...

BASI LAUA LAJERUHI MKOANI RUKWA

MTOTO mwenye umri wa miaka minne amefariki dunia papo hapo baada ya basi lenye Namba za usajili  T178 DHD lililokuwa likisafiri kutoka Kabwe wilayani Nkasi kuelekea mjini Sumbawanga mkoani Rukwa kuacha njia na kupindukaa huku abiria 25 wakijeruhi na tisa kati yao wakiwa ni majeruhi. Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Kabwe  Jofrey Kuzumbi alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Mei 5 majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la Malimba katika kata hiyo ya Kabwe. Alisema gari hilo lilikua limebeba  abiria 43 na waliojeruhiwa ni 25 na kati yao tisa ni mahututi na wamekimbizwa katika hospitali teule ya wilaya Nkasi huku wengine wakipelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa kwa matibabu zaidi kutokana na majeraha waliyoyapata. Alisema baada ya ajali hiyo kutokea mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Beatrice Nyansio (4) alifariki papo hapo huku mzazi wake akipata majeraha. Afisa mtendaji huyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi hilo n...

MSITU WA TONGWE MAGHARIBI WENYE SOKWE ZAIDI YA 800 SASA MIKONONI MWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Muhando akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katuma(PICHA NA Issack Gerald) Sokwe moja ya wanyama wanaopatikana msitu wa Tongwe Magharibi Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Kapanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Mpanda Salehe Muhando(Hayupo pichani)(PICHA NA Issack Gerald) Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na utalii imekubali msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kutoka katika mamlaka ya wizara hiyo. Muhando amebainisha hatua hiyo kupitia mikutano ya hadhara katika vijiji vya Kapanga na Katuma Kata ya Katuma lengo likiwa ni kuelimisha kutunza msitu huo wenye zaidi ya sokwe 800 kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA KIFO CHA MARIA NA CONSOLATA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameungana na Watanzania kuomboleza msiba wa watoto Maria na Consolata,waliofariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya mkoa wa Iringa. Rais Magufuli katika ukurasa wake wa Twitter ametuma ujumbe akielezea kusikitishwa kwake na msiba wa watoto hao ambao hivi karibuni aliwatembelea walipokuwa hospitali ya Muhimbili wakipatiwa matibabu hivi karibuni. Vifo hivyo vimetokea siku chache baada ya kuruhusiwa kutoka Hospotali ya Taifa Muhimbili ambako walikuwapo zaidi ya miezi miwili wakipatiwa matibabu. Taarifa kutoka Hospitali mkoani Iringa zinaeleza kuwa watoto hao walifariki kwa muda tofauti ambapo mmoja alifariki saa 1 usiku na mwengine alifariki saa 3 usiku. Maria na Consolata ambao ni pacha walizaliwa hapa nchini wakiwa wameungana na wakaishi hadi kujiunga na chuo kikuu wakiwa bado wameungana. Pacha hao waliokuwa na umri wa miaka 22 wamekuwa wakitunzwa na watawa wa kanisa Katoliki tangu na baada ya kuza...

ASASI ZA KIRAIA ZAINGILIA KATI SUALA LA KUONDOLEWA WALIMU WA ELIMU MAALUMU SHULENI AZIMIO

Image
Asasi za kiraia Mkoani Katavi zimelazimika kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ili kuzungumza naye kuhusu hatua ya kuwaondoa walimu waliokuwa wakifundisha watoto wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Azimio bila kuweka wengine mbadala. Asasi hizo zimesema katika kipindi cha mwaka 2015 mpaka sasa wanafunzi wenye ulemavu hawafundishwi masomo inavyotakiwa baada ya walimu watatu kati ya watano wa elimu maalumu waliokuwepo kuondolewa katika shule hiyo na kupangiwa majukumu mengine. Zimesema,walimu watatu walioondolewa shuleni walipandishwa madaraja kuwa walimu wakuu katika shule zisizokuwa na watoto wenye ulemavu,mwingine akipandishwa daraja na kuwa mratibu elimu maalumu katika Manispaa ya Mpanda ambapo mpaka sasa amebaki mwalimu mmoja anayefundisha darasa la kwanza mpaka la saba. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu amesema hakuwa na taarifa ya kuondolewa kwa walimu hao...

NKASI KINARA WA MIMBA KWA WANAFUNZI MKOANI RUKWA

Afisa serikali za mitaa mkoani Rukwa Bw.Albinus Mgonya amesema halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani humo ndiyo inayoongoza kwa wanafunzi kupata ujauzito mkoani Rukwa. Mgonya amebainisha hali hiyo kupitia kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi katika halmashauri hiyo. Katika kipindi cha miezi tisa jumla ya wanafunzi 74 wamekatiza masomo kutokana na kupata ujauzito ambapo kwa mjibu wa katika takwimu hiyo,wanafunzi 36 ni wanafunzi wa shule za msingi na wanafunzi 38 wa sekondari waliopata ujauzito huo kuanzia Julai mwaka jana mpaka Aprili mwaka huu. Alisema kulingana na takwimu hizo,wanafunzi wanaopata ujauzito ni sawa na kuwa kila mwezi wanafunzi   wanne wa shule za msingi   wanapata ujauzito sambamba na wanne wa sekondari wanapata ujauzito. Kutokana na hali hiyo,Mgonya ameiagiza halmashauri ya wilaya Nkasi kuandaa taarifa itakayoainisha idadi ya Watoto wenye mimba,mahali walipo wazazi   wao ikiwa ni pamoja na viongozi wa maeneo yao hasa Watendaji wao wa ...

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

Image
Abdulrahman Kinana alizaliwa mwaka 1952 mkoani Arusha Arusha Kaskazini mwa Tanzania. Kinana ni mwanasiasa aliyeshika nyadhifa mbalimbali serikalini. Alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani akibobea kwenye masuala ya mikakati. Alikuwa Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa ,naibu Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimatafa na Waziri wa ulinzi. Kinana aliwahi kufanya kazi na Jeshi la wananchi la Tanzania kwa miaka 20 kabla ya kusaafu akiwa na cheo cha ukanali mwaka 1972. Abdulrahman Kinana pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Afrika mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED