Posts

RC RUKWA AFANIKISHA ENEO LA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amefanikisha kupatikana kwa ekari 3 ili kujengwa kwa nyumba za askari polisi katika eneo la karibu na kituo cha polisi kipya kinachomaliziwa kujengwa katika kata ya Mtowisa,Wilayani Sumbawanga na kurahisisha makazi ya polisi katika bonde la ziwa Rukwa. Hayo yamejiri ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya wananchi wa kata ya Mtowisa kwa Mkuu wa Mkoa waliyoiahidi tarehe 13.11.2017 Mh.Wanagabo alipofanya ziara katika eneo hilo na kudai kuwa usalama wa bonde hilo sio mzuri kwa kukosa kituo bora cha polisi na makazi yao na kupelekea kuanzisha ujenzi wa kituo na hatimae kuomba nguvu ya Mkuu wa Mkoa kuweza kumalizia ujenzi huo. Mtendaji wa Kata ya Mtowisa Paulo Katepa alimuhakikishia MKuu wa Mkoa kuwa eneo hilo limeshapatikana na tayari kwa kukabidhi kwa askari polisi kwaajili ya taratibu nyingine za kisheria na kumuhakikishia kuwa eneo hilo halihitaji fidia ya aina yoyote na kwamba wananchi wa Kijiji cha Mtowisa wameridhia bila ya kusukumwa, na ...

WAKAZI WALALAMIKA KITUO CHA AFYA KUKOSA CHUMBA CHA KUHIFAHIDHIA MAITI

Image
WAKAZI wa kata ya mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wamelalamikia kitendo cha kituo cha afya Mtowisa ambacho ni kikongwe kwa zaidi ya miaka 20 kutokuwa na chumba cha kuhifadhia maiti kitendo kinachosababisha wagonjwa kukaa na maiti muda mrefu wodini baada ya mtu kufariki. Wakizungumza mbele ya mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi na kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.  Wakazi hao walimweleza mkuu huyo wa mkoa kuwa wagonjwa wanalazimika  kulala na miili ya marehumu wardini  huku wakisubiri ndugu wa marehamu kufika na kuchukua miiili hiyo kwa maziko na wakati mwingine maziko ya baadhi ya watu yamekuwa yakifanyika haraka bila kusubiri ndugu wa karibu na marehemu hao kutokana na kuzikwa mapema kwa kuhofia kuharibika kutokana na  kukosekana chumba cha kuhifadhia maiti. Mmoja wa wakazi hao  Christina Mponji alisema kuwa iwapo kifo kikimfika mgonjwa aliyekuwa amelazwa jirani na kitanda ch...

MAHAKAMA KUTOA HUKUMU KESHO MKOANI KATAVI

Image
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Mh.Chigangwa Tengwa amesema kesho Aprili 10,2018 inatarajia kutolewa hukumu dhidi ya Kigalu Huba mkazi wa kijiji cha Kambuzi Halt wilayani Mpanda Mkoani Katavi anayekabiliwa na kosa la kukutwa na risasi 12 za silaha aina ya kivita   ya AK47. Mh.Tengwa amefikia uamuzi huo leo baada ya kusikiliza mashahidi wa pande zote mshtaki na mshtakiwa. Awali mkuu wa mpelelezi mkoani Katavi Emmanuel Parangyo ameiambia mahakama hiyo kuwa Bw.Humba alipatikana na hatia hiyo Tarehe 19 Machi,2018   katika nyumba anayoishi. Aidha Parangyo ameiambia mahakama kuwa mwananchi haruhusiwi kumiliki risasi au silaha ya kivita kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi ya Tanzania. Mmoja wa mashuhuda upande wa washtaki akiwemo Mwenyekiti wa kijiji cha Kambuzi Halt Bw.Tuamin Elly,Bw.Huba alikuwa akilalamikikiwa na wananchi kwa kujihusisha na matukio ya uhalifu mara kwa mara. Hata hivyo mtuhumiwa amekana mashtak...

MAOFISA WA JESHI LA POLISI 458 WATIMULIWA KAZI

Image
Jumla ya maofisa wa Jeshi la Polisi wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa jana Aprili 7 na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa akizungumza mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za Polisi na ufunguzi wa kituo cha Polisi cha Utalii na Kidiplomasia jijini Arusha. Sirro alisema kazi ya Jeshi la Polisi ni kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza. Alifafanua kwa kulitambua hilo ndiyo maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015, 198 walifukuzwa kazi. Alisema kwa mwaka 2016 walifukuzwa askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa askari 14. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

POLISI RUKWA WAANZISHA OPARESHENI KUSAKA MASHAMBA YA BANGI.

Image
Jeshi la Polisi katika wilaya ya Kipolisi ya Raela Mkoani Rukwa limeanzishaa Oparesheni ya Kuyasaka mashamba yanayolima zao haramu ya bangi katika safu ya milima ya Lyamba Lyamfipa kwenye bonde la ziwa Rukwa. Mkuu wa Polisi katika wilaya hiyo ya kipolisi ya Raela Mrakibu mwandamizi wa polisi Aloyce Nyantola akizungumza leo wakati akishuhudia vijana kutoka kata ya Kapenta wilayani Sumbawanga wakivuna shamba la bangi lenye ukubwa wa heka 2 amesema walipata taarifa za kilimo hicho kutoka kwa raia wema na ndipo walipoanza kuzifanyia kazi. Katika Oparesheni hizo Nyantola ametoa wito kwa wananchi kuwa wema kuendelea kutoa taarifa huku akiwtaka pia kuzingatia sheria za nchi   na kuachana na kilimo cha mazao haramu. Kwa upande wake mkuu wa upelelezi wa wilaya hiyo ya kipolisi ya Raela mrakibu msaidizi Beda Msola amesema wananchi hao wamekuwa wakiendesha kilimo cha madawa ya kulevya ikiwemo bangi katika milima ya safu ya milima ya lyamba lyamfipa kwa kigezo kuwa maeneo ya msituni ...

RAIS MAGUFULI ASISITIZA SERIKALI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA DINI KULETA MAENDELEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika masuala mbalimbali ya maendeleo hapa nchini. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika Ibada ya kumsimika Mhashamu Askofu Isaac Amani kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la MtakatifuTeresia wa Mtoto Yesu Jijini Arusha. Mhashamu Askofu Isaac Amani aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francis tarehe 27 Desemba,2017 kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo na amesimikwa na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa Baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Marek Solczynski. Hatua ya rais Rais Magufuli kuhudhuria ibada hii ya kanisa katoliki imechukuliwa kama ishara bora ya kurejesha uhusiano mwema na baadhi ya makanisa makuu ya kikristo likiwemo kanisa katoliki ambao wamekua wakiikosoa vikali serikali yake....

AJALI YA BODABODA NA GARI KATAVI

Image
Dereva wa pikipiki maarufu kama Boda boda ambaye  jina lake halikufahamika Mara Moja Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,amejeruhiwa baada ya pikipiki yenye namba za usajil Mc 743 BQG aliyokuwa akiendesha kuligonga kwa Nyuma gari aina ya Raum eneo la Buzogwe njia mbili. Mashuhuda wa tukio hilo  ambalo limetokea leo wamesema,dereva huyo alikuwa akijaribu kuingia barabara kuu ya Buzogwe ndipo akawa amegongana na  Gari lenye namba za usajili T498 CFU.  Kwa mjibu wa mashuhuda hao,madereva wote wawili walikuwa na makosa baada ya wote kutozingatia sheria za usalama barabarani. Hata hivyo dereva wa gari hilo ambalo limegongana na pikpiki ametokomea kusikojulikana baada ya kutoonekana eneo la tukio baada ya Ajali hiyo kutokea. Hata hivyo askari polisi wa usalama barabarani ambao walifika eneo la tukio,wamekataa kuzungumzia tukio hilo wakidai wao siyo wasemaji. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com