MAHAKAMA KUTOA HUKUMU KESHO MKOANI KATAVI
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya hakimu
mkazi wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Mh.Chigangwa Tengwa amesema kesho Aprili 10,2018 inatarajia kutolewa hukumu dhidi ya Kigalu Huba mkazi wa kijiji cha Kambuzi Halt
wilayani Mpanda Mkoani Katavi anayekabiliwa na kosa la kukutwa na risasi 12 za
silaha aina ya kivita ya AK47.
Awali mkuu wa mpelelezi mkoani Katavi
Emmanuel Parangyo ameiambia mahakama hiyo kuwa Bw.Humba alipatikana na hatia
hiyo Tarehe 19 Machi,2018 katika nyumba
anayoishi.
Aidha Parangyo ameiambia mahakama
kuwa mwananchi haruhusiwi kumiliki risasi au silaha ya kivita kwa kuwa kufanya
hivyo ni kinyume na sheria za nchi ya Tanzania.
Mmoja wa mashuhuda upande wa washtaki
akiwemo Mwenyekiti wa kijiji cha Kambuzi Halt Bw.Tuamin Elly,Bw.Huba alikuwa
akilalamikikiwa na wananchi kwa kujihusisha na matukio ya uhalifu mara kwa
mara.
Hata hivyo mtuhumiwa amekana mashtaka
dhidi yake ya kumiliki risasi hizo bila kibali.
Aidha ameiomba mahakama impunguzie
adhabu atakapobainika kuwa na hatia kwa kuwa anategemewa na familia yake pamoja
na mama yake mzazi ambaye kwa sasa ni mgonjwa akimtegemea pia.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments