WAKAZI WALALAMIKA KITUO CHA AFYA KUKOSA CHUMBA CHA KUHIFAHIDHIA MAITI
WAKAZI
wa kata ya mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wamelalamikia kitendo cha
kituo cha afya Mtowisa ambacho ni kikongwe kwa zaidi ya miaka 20 kutokuwa na
chumba cha kuhifadhia maiti kitendo kinachosababisha wagonjwa kukaa na maiti
muda mrefu wodini baada ya mtu kufariki.
Wakizungumza
mbele ya mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi
na kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.
Wakazi
hao walimweleza mkuu huyo wa mkoa kuwa wagonjwa wanalazimika kulala
na miili ya marehumu wardini huku wakisubiri ndugu wa marehamu
kufika na kuchukua miiili hiyo kwa maziko na wakati mwingine maziko ya baadhi
ya watu yamekuwa yakifanyika haraka bila kusubiri ndugu wa karibu na marehemu
hao kutokana na kuzikwa mapema kwa kuhofia kuharibika kutokana na
kukosekana chumba cha kuhifadhia maiti.
Mmoja
wa wakazi hao Christina Mponji alisema kuwa iwapo kifo
kikimfika mgonjwa aliyekuwa amelazwa jirani na kitanda chako hali
inayosababisha kupatwa na hofu jambo linalosababisha kutoroka hospitali kabla
huduma za matibabu hazijakamilika.
Naye Msafiri
Malema alisema kukosekana kwa chumba cha kuhifadhia maiti jambo hilo
limetokana na uongozi wa kata kutokuwa na hamasa ya kuwahamasiasha wananchi
kujitokeza katika nguvukazi ya ujenzi wa chumba hicho kitendo ambacho
kingeondowa changamoto hiyo.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa huo Wangabo aliwataka wakazi wa kata hiyo kuanza
mara moja nguvu kazi kwaajili ya ujenzi wa huku akiwaahidi kutoa
bati wa watakapokuwa wamekamilisha ujenzi wa chumba hicho cha akuhifadhia
maiti
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments