Posts

MTANZANIA AHUKUMIWA KUNYONGWA UGANDA

Image
Mahakama Kuu nchini Uganda imemuhukumu Mtanzania kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji. Mtanzania huyo aliyetambulika kwa jina la Matule Chresporeto Coleheri mkazi wa Bukoba anadaiwa kumuua mfanyakazi mwenzake katika shamba moja lililoko eneo la Wakyuto wilayani Nakaseke. Akisoma hukumu hiyo,Jaji Steven Mubiru amesema baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka,mahakama imejiridhisha kuwa Matule ndiye alitenda kosa hilo. Amesema  mashahidi watatu walioshuhudia tukio hilo wameiridhisha mahakama kuwa Thomas Kamuhebwa aliuawa na mtuhumiwa huyo. Mwili wa Kamuhebwa ulikutwa ukiwa umetupwa katika shimo moja na kufungwa katika begi hali iliyosababisha mwili kuokotwa  karibu na makazi ya mshtakiwa. Hata hivyo,mbele ya mahakama hiyo Matule alijitetea kutohusika katika mauaji hayo na kudai tuhuma hizo zilitengenezwa na watu waliotaka kuiba magogo yake aliyoyaandaa kwa ajili ya kuzalisha mkaa. Awali,ilielezwa mahakamani hao kuwa Matule...

KIFO:MSANII RADIO AFARIKI DUNIA

Image
Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Radio amefariki dunia. Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel,tangu January 23 mwaka huu hali yake ilikuwa ikiripotiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana na ugomvi wa klabu. Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel,tangu January 23 mwaka huu hali yake ilikuwa ikiripotiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana na ugomvi wa klabu. Hapo jana Rais wa Uganda,Yoweri Museven alitoa Milioni 30 kwa ajili ya  matibabu ya msanii huyo pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika February 4 mwaka huu katika kanisa la Light the World. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MBUNGE ALIYESIMAMIA KIAPO CHA RAILA ODINGA AKAMATWA

Image
Mbunge wa Ruaraka Tom J Kajwang’ ambaye jana Jumanne alisimamia “kuapishwa” kwa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga kwenye viwanja vya Uhuru Park Jumanne amekamatwa. Mbunge huyo amekamatwa leo mchana na maofisa wa polisi ambao hawakuwa wamevalia sare nje ya Mahakama ya Milimani jijini Nairobi. Alikamatwa muda mfupi baada ya kuhudhuria katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji George Odunga kusikiliza uamuzi wa kesi aliyowawakilisha wabunge wanaopinga kukatwa mishahara yao na posho. Kajwang’ na mwanasheria mwingine Miguna Miguna,ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa matukio katika viwanja vya Uhuru Park yaliyomalizikia kwa “kuapishwa” Odinga kama ‘rais wa wananchi’. Wakati wa sherehe za kiapo Kajwang’ alikuwa amevaa vazi na wigi na alishangiliwa sana na wafuasi wa Nasa. Odinga alikula “kiapo” huku Kajwang’ akiwa amesimama nyuma yake japokuwa wajibu wake katika tukio hilo bado haujafahamika. Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED

RAIS MUSEVEN ATOA MILIONI 30 KUFANIKISHA MATIBABU YA RADIO

Image
Rais wa Uganda Yoweri Museven ametoa shilingi Milioni 30 kwa ajili ya  matibabu ya msanii Radio. Msanii Radio ambaye amekuwa akifanya kazi na mwenzake Weasel alipata ajali January 23 mwaka huu na hali yake inaripotiwa kuwa mbaya. Hapo jana taaarifa ilitolewa kupitia ukurasa wa Instagram wa Radio na Weasel ilieleza kuwa February 4 mwaka huu kutafanyika maombi maalumu kwa ajili ya kumuombea Weasel. Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA MZEE MAJUTO HOSPITALI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli amemtembelea muigizaji mkongwe,Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa. Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara. Pamoja na hayo,Mzee Majuto aliendelea kwa kusema ; “sisi wazee tunafarijika sasa hivi,viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko kwa uoga maana hataki masihara. Kwa upande mwingine, Mzee Majuto amesema sio rahisi kupata Rais mwenye misimamo na asiyekuwa na masihara kama Dkt.John Magufuli. Chanzo:Bongo5.com Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED