Posts

MWANAFUNZI AUAWAWA KIKATIRI POLISI KATAVI WAMSAKA MUUWAJI

Image
Na.Issack Gerald-Katavi JESHI la polisi mkoani Katavi linamsaka mtu asijejulikana kwa tuhuma za kumbaka,kumchoma kisu,kumuua na kisha kukata sehemu za siri za mwanafunzi(14) wa  darasa la sita shule ya msingi  Vikonge wilaya ya  Tanganyika na kukimbilia kusiko julikana. Akitoa taarifa ya tukio hilo kamanda wa polisi Damas Nyanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 1;30 za asubuhi wakati marehemu akiwa anakwenda shule akiwa ameongozana na mdogo wake ambaye wanasoma shule moja. Alisema kuwa siku ya  tukio hilo marehemu  alitoka  nyumbani akiwa na mdogo wake wa kiume  mwenye  umri wa miaka 11  mwanafunzi wa   darasa  la  nne  ambaye waliongozana wakielekea  shule ya  msingi  vikonge ambayo wanasoma. Kamanda Nyanda alisema wakiwa  njiani  alitokea  mwendesha  pikipiki maarufu kwa jina bodaboda  ambae walikuwa  hawamfahamu  na  kusimamisha...

BARAZA LA MADIWANI MPANDA LAONYA WATUMISHI WANAOSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI

Image
Na.Issack Gerald Baraza la Madiwani Halamshauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,limesema litachukua hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafukuza kazi watumishi wa idara ya ardhi watakaosababisha migogoro ya ardhi baina ya wananchi. Mstahiki Meya wa Manispaa Mpanda Mh.Willium Mbogo Tamko hilo ambalo limtolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Willium Mbogo kupitia kikao maalumu cha bajeti cha baraza hilo ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo. Amesema kumeanza kujitokeza migogoro ya ardhi kuhusiana na kiwanja kimoja kuuzwa kwa watu wawili tofauti suala ambalo limetajwa kufanywa na watumishi wa idara ya ardhi wasio waaminifu na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Willium Mbogo amelazimika kuagiza migogoro hiyo isuluhishwe wao kwa wao kabla ya tatizo kuwa na baraza kupewa taarifa. Aidha amesema hatua za kisheria zitachukuliwa pia kwa watumishi wa idara mbalimbali ambao wamesababisha Manispaa ya Mpanda Kukosa mapato kutokana na uzembe wao katika uwajibikaji...

GESI YA HELIUM YA FUTI ZA UJAZO BILIONI 98.9 YAGUNDULIWA MKOANI RUKWA

Image
Kampuni ya uchunguzi na utafiti wa madini Helium One, ambayo kwa sasa inafanya utafiti wa gesi ya heliamu mkoa wa Rukwa imegundua kuwapo kwa futi za ujazo bilioni 98.9 za gesi hiyo katika maeneo iliyokwishafanyia uchunguzi. Hayo yalielezwa katika warsha ya siku moja iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kuratibiwa na Idara ya Jiolojia ya chuo hicho Helium One na Chuo Kikuu cha Oxford. Akizungumza katika warsha hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Helium One,Thomas Abraham-James alisema kampuni yao imetafuta leseni 23 za uchunguzi na kwamba nyingine tatu zimeombwa. Alisema leseni hizo zote zinamilikiwa na kampuni hiyo kwa asilimia 100 na kwamba ina haki za kipekee za gesi hiyo ya heliamu . Pamoja na kutoa taarifa hiyo,alisema lengo la kuwa na warsha ni kuwaita wataalamu na wadau mbalimbali wa hapa nchini na kimataifa kubadilishana uzoefu na taarifa zilizopo kuhusu gesi hiyo na kuangalia fursa zinazoambatana na uwapo wa gesi hiyo katika harakati za kitaifa za kuwa na taifa...

MWANAFUNZI WILAYANI TANGANYIKA AUWAWA KIKATIRI

Image
Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi V ikonge K ata ya tongwe   wilaya ya Tanganyika mkoani katavi mwenye umri wa miaka 14 amefariki dunia baada ya kubakwa kisha kubakwa na kisha kutupwa porini . K amanda wa polisi mkoa wa K atavi Damas Nyanda  ameeleza kuwa tukio hilo limetokea tarehe 22 majira ya saa mbili asubuhi wakati msichana huyo akiwa na mdogo wake wa kiume kuelekea shuleni. Ameongeza kusema upelelezi unaendelea ilikuwabaini walio husika na kitendo hicho cha ukatili ili mkondo wa sheria uchukue nafasi yake . Wananchi wamegadhabishwa na kitendo hicho wengi wakilitaka jeshi la polisi kuwatia nguvuni wahalifu hao mara moja. Katika hatua nyingine kamanda huyo amekemea vikali kwa wale wote wanaomiliki silaha kinyume n a sheria akiwataka kuzisalimisha jeshi la polisi. Kwa mjibu wa kaka wa marehemu ambaye naye alikuwa mwanafunzi pamoja na wakazi wa kijiji cha Vikonge wamesema kuwa mwanafunzi huyo aliomba lifti kwa bodaboda na hivyo kubeb...

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME USO KWA USO NA TRUMP

Image
Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kukutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano wa masuala ya kiuchumi World Economic Forum (WEF) unaofanyika mjini Davos Uswizi. Kagame atakuwa kiongozi wa pekee wa bara Afrika anayetarajiwa kukutana na Trump kulingana na ratiba iliyotolewa na mshauri wa masuala ya kiusalama wa Marekani H.R McMaster. Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Ijumaa huku kukiwa na malalamishi makubwa dhidi ya Trump ambaye aliyataja mataifa ya Afrika kuwa machafu ambapo hata hivyo Trump Mwenyewe baadaye alikana madai hayo. Mkutano wa rais Trump na Kagame ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika utaimarisha uhusiano wa Afrika na Marekani na kuzungumzia masuala muhimu ikiwemo biashara na usalama. Muungano wa Afrika umemtaka rais Trump kuomba msamaha kwa matamshi yake ya kukera ambapo wakati huo huo Trump anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na rais wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Davos. Habari zaidi n...