Posts

RAIS MAGUFULI AOMBOLEZA KIFO CHA JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof.Ibrahim Hamis Juma kufuatia kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe.Robert Kisanga kilichotokea jana. Rais Dkt.John Magufuli Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais IKULu Gerson Msigwa Marehemu amefariki jana katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam. Katika salamu hizo Mhe.Rais Magufuli amesema Jaji Mstaafu Robert Kisanga atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa wakati wote wa utumishi wake uliojaa umakini,uchapakazi,uzalendo na ushirikiano. Aidha Mhe.Rais Magufuli amewaombea wafiwa wote wawe na moyo wa subira,uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea Marehemu Jaji Mstaafu Kisanga apumzishwe mahali pema peponi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

UHARIFU MTANDAONI SASA MPAKA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MPANDA

Image
Wananchi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kuwa makini wanapofanya miamala yoyote ya pesa kwa watu wasiowafahamu vizuri ili kutokomeza utapeli wa pesa kimtandao ambao umeshamiri Mkoani Katavi. Wito huo umetolewa na Afisa wa Polisi kutoka Ofisi ya Upelelezi Wilayani Mpanda Thobias Lindege ambapo ametoa elimu ya kupambana na uharifu wa kimtandao elimu ambayo ameitoa kupitia baraza maalumu la madiwani la Manispaa ya Mpanda. Aidha Lindege amewataka wananchi Mkoani Katavi kutonunua simu ovyo kutoka kwa watu bila utaratibu kwa kuwa inapobainika simu hiyo imetumika kiuharifu,aliyenunua simu hiyo naye huambatanishwa kama mharifu na hivyo kuwajibika katika kosa lililotendeka. Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Mbogo amesema wanatarajia kufuatalia wa matangazo yanayobandikwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda yakiwemo yanayohusisha waganga wa jadi lengo likiwa ni kutokomeza utapeli katika Manispaa ya Mpanda. Baadhi ya njia ambazo zime...

RAIS ASHTUSHWA NA KIFO ATUMA SALAAMU ZA RAMBIRAMBI

Image
Marehemu Jumanne Ntambi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Jumanne Ntambi na wachezaji wa Mwadui kwa kuondokewa na kocha wao usiku wa kuamkia leo huku akiwataka wafiwa wawe na moyo wa subira Rais Karia amesema hayo katika salamu zake zilizotolewa rasmi na Shirikisho hilo huku akisema ameshtushwa kupata taarifa hizo kwani marehemu Ntambi alikuwa na mchango mkubwa katika soka la Tanzania. Enzi za uhai wake Jumanne Ntambi aliwahi kufundisha timu za Kahama United ya Shinyanga, Mlale JKT ya Ruvuma, Panone ya Kilimanjaro,timu ya mkoa wa Shinyanga Igembe Nsabo na mpaka mauti yanamkuta alikuwa akiifundisha Mwadui ya Shinyanga akiwa kocha msaidizi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MWANAKWAYA MKOANI RUKWA AFARIKI BAADA YA KUTOA SADAKA

Image
Mwanakwaya wa kwaya ya Mtakatifu Secilia,Kigango cha Muze Parokia ya Zimba,Jimbo Katoliki Sumbawanga,Flora Nandi (25) ameanguka na kufariki dunia muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya shukrani akiwa kanisani. Tukio hilo limetokea siku ya  Jumapili  saa nne za asubuhi wakati wa ibada ya kwanza,kwaya ya Mtakatifu Secilia  ikimsifu Mungu katika ibada hiyo. Akizungumzia tukio hilo,mwalimu wa kanisa aliyekuwa akiongoza ibada hiyo,Katekista Philipo Lupadasi amesema wanakwaya wakiwa wanaimba na marehemu akiwa ametoka kutoa sadaka ya shukrani na kuendelea kuimba ghafla alianguka chini hali iliyozua mshtuko na kusababisha ibada kusimama kwa muda. Amesema baada ya kufikishwa katika zahanati hiyo alipokewa na wahudumu wa afya ambao baada ya kumfanyia uchunguzi walibaini kuwa alikuwa ameshafariki dunia. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOANI KATAVI LAKIRI KUSHINDWAA KUWANASUA WALIONASA MGODINI

Image
Miili ya vijana wawili waliofunikwa na kifusi cha udongo katika machimbo ya dhahabu yaliyo kijiji cha Ibindi  Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi bado haijaopolewa kwa wiki ya pili sasa. Kwa upande wa mashuhuda wa ajali hilo katika eneo la Kwa Songoro lililopo kijiji cha Ibindi wameelezea kusikitishwa na tukio hilo. Kwa mujibu wa mashahidi mmoja ya vijana waliopoteza maisha Azam Lawrence Nyembeke mkazi wa Iringa  ndugu zake hawana taarifa mpaka sasa. Licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na wachimbaji wakishirikiana na wananchi wa eneo hilo Jeshi la zimamoto na Uokoji mkoani katavi limekiri kushindwa kutoa miili hiyo kwa madai ya   ukosefu wa vifaa kazi vinavyowezesha kurahisisha uokoaji huo. Uchimbaji wa madini ni moja kati ya shughuli ianyowakusanya vijana kutoka mikoa mbali nchini lakini wakiwa katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kutokana na teknolojia duni ya uchimbaji. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED