Posts

MOROCCO YAZINDUA KAMPENI YA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA 2026

Image
Morocco imezindua kampeni yake ya kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya 2026 mjini Casablanca. Morocco imezindua kampeni yake ya kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya 2026 mjini Casablanca. Taifa hilo la Afrika kaskazini ambalo limewasilisha ombi lake la tano kuandaa fainali hizo,linakabiliwa na ushindani mkali kutoka ombi la pamoja linaloshirikisha Canada,Mexico na Marekani. Mwenyekiti wa ombi hilo Moulay hafid Elalamy amesema Morocco itaonyesha mchezo mzuri zaidi katika kombe hilo la dunia. Uamuzi wa atakayeandaa kombe hilo unatarajia utafanywa juni 13 mwak huu katika mkesha wa kombe la dunia la mwaka 2018 mjini Moscow. Taifa hilo la Afrika kaskazini limefeli katika maombi yake manne miaka 1994,1998,2006 na 2010. Mwaka wa 2010,mchuano huo uliandaliwa na Afrika Kusini huku bara hili likiandaa kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia. Morocco inataka kubadili hayo yote na imemteua Elalamy, waziri wa serikali kuongoza ombi hilo huku aliyekuwa katibu mkuu...

WAKAZI TABORA WATAKIWA KUACHA KUTUMIA DAWA KWA MAZOEA

Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wameshauriwa kujenga utamaduni wa kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuacha kutumia dawa kwa mazoea. Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa zahanati ya Moravian Milumbani,Dkt Lameck Kisulila amesema matumizi ya dawa bila utaratibu maalumu ni chanzo cha magonjwa nyemelezi mwilini na hata kusababisha vifo. Dkt.Kisulila ameitaka jamii kuwa na desturi ya kupima afya wanapougua kwa sababu itasaidia kubaini aina ya ugonjwa na tiba inayohitajika hatua itakayowasaidia kupunguza madhara mengine mwilini yanayotokana na usugu wa dawa. Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa mjini Tabora wamesema wanalazimika kutumia dawa bila kupima afya zao wanapougua kutokana na hali ngumu kiuchumi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAKULIMA MKOANI KIGOMA WAPEWA ELIMU YA KUENDESHA KILIMO BORA

Halmashuri ya Kigoma vijijini ikishirikiana na Shirika la maendeleo la vijana Tanzania la nyakitonto limeendesha semina ya kilimo cha mihogo,maharage na mahindi katika kata ya Nkungwe halmashuri ya Kigoma Ujiji. Kwa mjibu wa katibu washirika la Nyakitonto la mendeleo ya vijana wa Tanzania Teoneste Tereba amesema w akulima wengi wadogo wadogo wamekua na desturi za kulima kilimo cha mazoea kwa kutumia mbegu ambazo zisizokuwa na ubora ikiwa ni pamoja na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya mbolea jambo. Aidha Tereba amesema hali hiyo imesababisha itasaidia kuboresha kipato,uhakika wa chakula na hali za wakulima wa maharage mahindi na mhogo kwa mkoa wa kigoma kuwa katika ubora. Kwa upande wao Mikidadi Mbaruku ambaye afisa kilimo halmshauri ya Kigoma vijijini na Silyvesta Mchafu ambaye ni afisa kilimo kata ya Nkungwe wamesema watakuwa bega kwa began a wakulima hukuwa wakiwashauri wakulima kutumia elimu wanayopewa katika kuleta mabadiliko katika sekta ya kili...

MWAKA WA FEDHA 2018/2019 MANISPAA YA MPANDA KUKUSANYA ZAIDI YA BIL.26.8

Image
Na.Issack Gerald Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 26.8 katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo kati ya kiasi hicho mapato ya ndani yanarajia kuwa Shilingi bilioni 2.4. Hayo yamebainishwa na Afisa Mipango wa Manispaa hiyo Bi.Mary Luhulula wakati akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 kupitia kikao maalumu cha baraza la madiwani cha Manispaa ya Mpanda ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa. Aidha Bi.Luhulula pamoja na mambo mengine amesema mwaka 2017/2018 ilikusanywa shilingi bilioni 10.4 badala ya shilingi bilioni 27.4 iliyokuwa imeidhinishwa ambapo imepanga kubuni vyanzo vya mapato ili kupata fedha ili kuchochea maendeleo. Kwa upade wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Bw.Deodatus Kangu amesema baadhi ya tozo kurejeshwa serikali kuu ikiwemo kodi ya ardhi,mazao,mabango ya matangazo ya kijamii na baadhi ya ushuru kufutwa kumesababisha Hamlashauri ya Manispaa ya Mpanda kutofikish...

MTANGAZAJI MCHEZAJI AFARIKI DUNIA

Image
Mtangazaji na mchezaji mkongwe wa Uingereza mwenye heshima kubwa,Jimmy Armfield amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 82 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani. Jimmy Armfied mtanganzaji mkongwe Pamoja na kuichezea mechi 569 Timu ya Blackpool enzi zake, pia alikuwa Nahodha wa England mara 15 katika mechi 43 alizochezea Simba Watatu. Baada ya kuwa kocha wa timu za Leeds na Bolton, Armfield akahamia kwenye utangazaji na kujivunia heshima kubwa akiwa mchambuzi wa BBC Radio 5 Live. Na Familia yake imethibitisha kifo chake kilichotokea Trinity Hospice mapema asubuhi ya leo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED