ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 11 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA MANISPAA YA MPANDA
Jengo la Ofisi za Manispaa ya Mpanda na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi |
Na.Issack Gerald-Katavi
Zaidi ya shilingi bilioni 11,750,000,000 zimetengwa kwa ajili ya kuboresha barabara
katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.
Hatua hiyo imeelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda Enelia Lutungulu wakati wa
mkutano wa wadau wa mpango kabambe wa
Master plan ya miaka 20.
Lutungulu amesema fedha hiyo ni mpango wa uboreshaji
miundombinu ya Manispaa uitwao ULGSP uliopangwa kutekelezwa kwa
kipindi cha miaka mitano ambapo miradi saba imepangwa kutekelezwa katika
halmashauri 18 hapa nchini.
Aidha Lutungulu amesema mpango
wa uboreshaji wa miundo mbinu
katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ulianza tangu mwaka
wa fedha wa 2013/2014 na utakamilika mwaka wa fedha wa
2017 na2018.
Lutungulu ameitaja miradi saba iliyopangwa
kutekelezwa kwenye mradi huo kuwa ni usanifu wa miradi ya barabara
na ujenzi wa soko la kisasa katika Kata ya Kazima, ujenzi wa Stendi
ya mabasi ya kisasa katika eneo
la Ilembo, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu
wa kilometa 7.7 Mpanda Mjini na uandaaji wa mpango
kabambe wa Manispaa ya Mpanda na kujenga
uwezo.
Mradi huo utatekelezwa na mtaalamu mshauri
City Plan Consultancy T Limeted kwa gharama ya shilingi za
kitanzania 283 600,000 Fedha ambazo zimetolewa
na Manispaa ya Mpanda kupitia mpango wa utekelezaji
wa miji unaofdhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia.
Afisa Mipango miji
mshauri wa City Plan Consultancy T Limeted ya
Dar es salaam Bw.Iddy Mwerangi alisema ni lazima ziunganishwe nguvu
za wadau mbalimbali zitakazosaidia kupatikana kwa
taarifa mbalimbali zitakazowezesha uaandaaji wa mpango
Kabambe.
Naye Makamu Meya wa Manispaa ya Mpanda
John Matongo alisema swala hilo bila
ushirikiano wa wananchi haliwezi
kufanikiwa hivyo wao kama madiwani watahakikisha
zoezi hilo la mpango Kabambe
wa Master Plan linafanikiwa.
Kwaupande wake mkuu wa mkoa wa
Katavi Meja Jenerali mstaafu
Raphael Muhuga alisema kuwa mji
wa Mpanda unakuwa kwa hivyo ni vema
maeneo ya mji huo yakawa yamewekwa kwenye
mpango unaoeleweka.
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ni
miongoni mwa halmashauri hapa nchini zinazotekeleza miradi inayofadhiliwa na
benki ya dunia ambapo pamoja na Miradi mingine Halmashauri ya manispaa ya
Mpanda inaandaa mpango kabambe maarufu kama Master Plan utakaoongoza matumizi
ya ardhi ya manispaa ya Mpanda kwa kipindi miaka 20 ijayo.
Mpango
mchakato huo uliokuwa umeanza tangu mwaka 2010, haukufika mwisho kwa sababu ya
ongezeko la mahitaji ikiwa ni pamoja na ongezeko la ukubwa wa eneo la kiutawala
manispaa ya Mpanda hivyo kupelekea kuanza upya Mchakao huo kwa kuwa taarifa za
awali za msingi zilipitwa na muda wake.
Kwamujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Manispaa hiyo
ilikuwa na jumla ya wakazi 102,900 hivyo kupelekea kwenye mpango huo
kupata mgao wa Dola za kimarekani 7,342,975, ambazo
ni sawa na shilingi za kitanzania 11,750,000,000 ambazo zitatumika kutekelezwa
mpango huo kwa muda wa miaka mitano.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa
P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments