BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI,ATEUA PIA MAWAZIRI
Rais Dkt John Magufuli wa Tanzania |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,amefanya
mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
Tukio hilo limetokea leo ambapo Rais Magufuli pia amezigawa
Wizara ya Kilimo,Mifugo,Uvuvi na kuwa wizara ya Kilimo pekee na Wizara ya Mifugo
na Uvuvi peke yake,huku Wizara ya Nishati na Madini ikigawanya na kuwa wizara
mbili tofauti.
Sambaba na
hilo pia Rais Magufuli amemteua Mh. George Haruna Mkuchika kuwa Waziri
Ofisi ya Rais Utawala Bora,ambaye kabla ya kuteuliwa alikuwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge.
Kwa mabadiliko hayo wizara zimeongezeka kutoka 19 zilizokuwepo na hivyo
kufikia wizara 21.
Mawaziri hao wanatarajiwa kuapishwa siku ya jumatatu Oktoba 9,Ikulu
jijini Dar es salaam.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited
Group
Comments