ORODHA KAMILI YA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI WA RAIS MAGUFULI ALILOTANGAZA LEO
Na.Issack Gerald-Mpanda
Katavi
Rais Dkt John Magufuli wa Tanzania |
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya
mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kuongeza idadi ya Wizara, kuteua
Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya na kuwahamisha Wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu
Mawaziri.
Katika mabadiliko hayo
Mhe.Rais Magufuli ameongeza idadi ya Wizara na Mawaziri wake kutoka 19 hadi 21,
na Naibu Mawaziri kutoka 16 hadi 21.
Iliyokuwa Wizara ya
Nishati na Madini imegawanywa na kutakuwa na Wizara ya Nishati na Wizara ya
Madini na iliyokuwa Wizara Kilimo,Mifugo na Uvuvi imegawanywa na kutakuwa na
Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mhe.Rais Magufuli akiwa
na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa
Majaliwa ametangaza mabadiliko hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam na lifuatalo ni
Baraza la Mawaziri baada ya kufanyiwa mabadiliko.
1.Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora-Waziri –George Huruma
Mkuchika
2.Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Waziri Selemani Said Jafo,Naibu Waziri-Joseph
Sinkamba Kandege,Naibu Wazri -George Joseph Kakunda
3.Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Waziri January Yusuf
Makamba,Naibu Waziri -Kangi Alphaxard Lugola
4.Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu-Waziri -Jenista Joackim
Mhagama,Naibu
Waziri Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira),Naibu
Waziri - Stella Alex Ikupa (Walemavu)
5.Wizara ya Kilimo Waziri -Dkt. Charles John Tizeba,Naibu Waziri -Dkt.Mary
Machuche Mwanjelwa
6.Wizara ya Mifugo na Uvuvi- Waziri Luhaga Joelson Mpina,Naibu Waziri - Abdallah Hamis Ulega
7.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Waziri Prof.Makame
Mbarawa Mnyaa,Naibu Waziri-Mhandisi Atashasta Justus Nditiye,Naibu
Waziri-Elias John Kwandikwa
8.Wizara ya Fedha na Mipango Waziri-Dkt. Philip Isdor Mpango,Naibu Waziri -Dkt. Ashatu Kijaji
9.Wizara ya Nishati-Waziri Dkt.Medard Matogoro Kalemani,Naibu Waziri -Subira
Hamis Mgalu
10. Wizara ya Madini-Waziri
-Angellah Kairuki,Naibu Waziri -Stanslaus Haroon Nyongo
11.Wizara ya Katiba na Sheria,Waziri-Prof. PalamagambaJohn
Aidan Mwaluko Kabudi.
12. Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki-Waziri -Dkt. Augustine Philip Mahiga,Naibu
Waziri -Dkt. Susan Alphonce Kolimba
13. Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Kujenga (JKT)-Waziri Dkt. Hussein Ali Mwinyi
14. Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi-Waziri
Mwigulu Lameck Nchemba,Naibu Waziri-Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
15. Wizara ya Maliasili
na Utalii-Waziri-Dkt.Hamisi Andrea Kigwangalla,Naibu Waziri-Josephat Ngailonga
Hasunga
16.Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi-Waziri William Vangimembe Lukuvi,Naibu
Waziri- Angelina Sylivester Mabula
17.Wizara ya Viwanda,Biashara
na Uwekezaji,Waziri-Charles Paul Mwijage,Naibu Waziri-Mhandisi Stella Martin
Manyanya
18.Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia
na Ufundi-Waziri Prof. Joyce Lazaro Ndalichako,Naibu Waziri-William Tate Ole
Nasha
19.Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Waziri-Ummy Ally Mwalimu,Naibu
Waziri - Dkt.Faustine Engelbert Ndugulile
20.Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo-Waziri -Dkt. Harrison George Mwakyembe,Naibu Waziri Juliana Daniel
Shonza
21.Wizara ya Maji na
Umwagiliaji-Waziri Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe,Naibu Waziri - Jumaa
Hamidu Aweso
Wakati huo huo,Mhe.Rais Magufuli
amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Kabla ya Uteuzi huo,Bw.Stephen
Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.
Bw.Stephen Kagaigai
anachukua nafasi ya Dkt.Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wateule wote wanatarajia
kuapishwa Jumatatu ya Oktoba 9,2017 saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited
Group
Comments