WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO YATOA TAARIFA KUHUSU SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE KITAIFA
Na.Issack Gerald
Mkoa wa
Katavi umeendelea kutajwa kuwa kinara wa mimba za utotoni kwa asilimia 45.
Hayo
yamebainishwa Mkurugenzi wa
Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi Magreth Mussai wakati akizungumza na waandishi
wa habari Mjini Dodoma,kuhusu Maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Mtoto
wa Kike duniani.
Bi Magreth Mussai ametaja mikoa mingine
inayoongoza kuwa mimba za utotoni baada ya Mkoa wa Katavi kuwa ni Tabora
(43%),Dodoma (39%),Mara (37%) na Shinyanga (34%).
Katika hatua nyingine taarifa ya
utafiti ya hali ya ukatili dhidi ya watoto iliyotolewa mwaka 2011,inaonyesha
kwa kila watoto wa kike 3 mtoto 1 sawa na asilimia 27.9 amefanyiwa vitendo
vya ukatili huku takribani asilimia 6.9 wakilazimishwa kufanyiwa ukatili wa
kingono.
Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika
siku ya mtoto wa kike duniani ni pamoja na kutoa elimu ya kujitambua
na afya ya uzazi ili watoto wa kike wajilinde na mimba za utotoni.
Kabla ya maadhimisho hayo,kutakuwepo Kongamano la
Wazazi,walezi,viongozi wa dini na watu mashuhuri watakaojadili changamoto za
malezi kwa mtoto.
Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka
2014 inaonyesha kuwa asilimia 11 ya wanawake waliojifungua walikuwa na umri
kati ya miaka 15 -19 .
Wakati huo huo Utafiti wa Afya ya Uzazi na Utoto na
Viashiria vya Malaria (TDHS) wa mwaka 2015 unaonyesha asilimia 27% ya watoto wa
kike wanapata mimba wakiwa na umri chini ya miaka 18.
Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazowakabili watoto wa kike Serikali kwa kushirikiana na wadau imeanza
kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake
na Watoto (2017/2018 -2021/2022).
Mpango huu umelenga kupunguza ukatili dhidi ya
watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/22 na tunatarajia kupunguza mimba za
utotoni kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia 5.
Maadhimisho hayo yatakayofanyika kitaifa Mkoani mara
Oktoba 11 mwaka huu,yatakuwa na kaulimbiyu isemayo‘’Tokomeza Mimba za
Utotoni; Tufikie Uchumi wa Viwanda’’.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments