HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO YAKABIDHI MSAADA WA BAISKELI 20 ZENYE THAMANI YA MILIONI 11 KWA WATU WENYE ULEMAVU
Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
HALMASHAURI ya Wilaya ya Nsimbo
Mkoani Katavi,imekabidhi msaada wa baiskeli ishirini za tairi tatu zenye thamani
ya shilingi milioni kumi na moja kwa watu wenye ulemavu katika halmashauri hiyo.
Akikabidhi msaada huo kaimu
mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Frednandi Filimbi pamoja na mambo mengine ameitaka jamii
kutowaficha watu wenye ulemavu ili wapate haki zao stahiki.
Aidha Bw.Filimbi amesema kwa sasa
Halmshauri inatafuta fedha ili kujenga bweni katika mojawapo ya shule
itakayochaguliwa ndani ya Halmshauri ili kuwajengea mazingira ya watoto kusoma
wakitokea katika eneo moja.
Kwa upande wake Afisa ustawi wa Jamii
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi.Dianarose Mnuo,ameonya watu wasiohusika
wakiwemo watu wakubwa na watoto kuchezea baiskeli ambazo zimetolewa maalumu kwa
watu wenye ulemavu.
Mwakilishi wa kampuni ya uwindaji wanyama
hapa nchini Conservation Foundation Tanzania (CFT) Bi.Rose Beker ambao ndiyo
wamekabidhi msaada huo kwa Halmashauri ya Nsimbo,amesema wataendelea kutoa
msaada katika maeneo mbalimbali Mkoani Katavi.
Kwa mjibu wa Afisa elimu Maalumu
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Clevery Mngao,Halmashauri watu wenye ulemavu
105 waliokwishawabaini wanaohitaji kupata msaada.
Nao baadhi ya wanuafaika wa msaada
huo akiwemo Elias Michael ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule
ya Msingi Mtambo amesema baiskeli hiyo itamsaidia
kumrahishia safari wakati wa kwenda shule huku wazazi na wakiomba makampuni
mengine kuiga mfano wa kampuni hiyo kwa kutoa msaada zaidi kwa makundi maalumu.
Watu hao wenye ulemavu waliokuwa
mchanganyiko wa watoto,wazee,vijana wanawake kwa wanaume wanatoka katika maeneo
kata mbalimbali za Halmshauri ya Wilaya Nsimbo.
Watu hao 20 waliopatiwa msaada ni
miongoni mwa watu wenye ulemavu 49 ambao Halmashauri ilikuwa imewaombea msaada.
Comments