ASKARI WA WANYAMAPORI MKOANI KATAVI WATUHUMIWA KUUWA NA KUJERUHI
MTU mmoja amepoteza maisha kwa madai ya kupigwa
risasi na askari wa maliasili na wengine
wanne kujeruhiwa katika kitongoji cha Mnyamasi wilayani
Tanganyika mkoani Katavi,wakati wa oparesheni ya kuwaondoa wakazi wanaodaiwa
kuvamia msitu wa hifadhi
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kitongoji cha Mnyamasi
Bw.Magosha Mtoveka amesema tukio hilo ambalo lilianza juzi na kuendelea mpaka
jana pamoja na askari hao wa maliasili kupiga ovyo risasi za moto pia vyakula
na mali nyingine inaelezwa zimechomewa ndani ya nyumba zao.
Awali imedaiwa askari walifika kijijini hapo na
kuanza kuwafurusha wakazi wa eneo hilo kwa kutumia nguvu na silaha za moto kwa
madai kuwa wamevamia hifadhi ya msitu wa Msaginya.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mpanda Dokta
Theopista Elisa amekiri kupokea majeruhi kadhaa hospitalini hapo japo hakutaka
kuthibitisha kuwa majeruhi hao wametokana na oparesheni hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi
mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka
wananchi kuwa na utulivu
Miezi ya hivi karibuni maeneo mbalimbali ya mkoa wa
katavi yamekuwa yakikumbwa na aina kama hii ya matukio hali amabyo mamlaka za
serikali zinadai zinatimiza majukumu yake.
Comments