WAKULIMA WAMESHAURIWA KUWEKA KIPAUMBELE KILIMO CHA MAZAO YA CHAKULA
Na.Issack
Gerald-Mpanda Katavi
Wakulima wametakiwa kuyapa kipaumbele
mazao ya chakula katika msimu wa huu wa kilimo ili kuwa na uhakika wa chakula
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya
Mpanda Bi Lilian.
Matinga wakati akihutubia mkutano wa
ufunguzi wa msimu wa kilimo ulifanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi
kakese
Bi matinga amesema kuwa ili kuweza
kupiga vita njaa wananchi wote hawana budi kulima kwa nguvu zao zote ili
kuhakikishia akiba ya kutosha ya chakula mwisho wa msimu
Katika hatua nyingine Bi Matinga
amewataka maafisa ugani kuwa na mashamba darasa ili yawasidie wakulima kulima
kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha kisasa
Baadhi ya wananchi waliohudhuria
mkutano huo wameishukuru hatua ya manispaakuzindua mradi huo katika kijiji chao
na kuwasogezea huduma za pembejeo za kilimo katika maeneo yao.
Comments