MADIWANI MANISPAA YA MPANDA WAMETOA TAMKO LA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UONGOZI WAKE
Na.Issack
Gerald-Katavi
Madiwani
wa Halmashauri ya Manispaa Mpanda
mkoani Katavi wamempongeza rais John Magufuli kwa ujasiri
aliouonesha wa kulinda rasilimali za
nchi hasa katika suala la madini.
Pongezi
hizo zilitolewa jana kupitia waandishi wa habari ambapo Meya wa Manispaa ya
Mpanda Willium Mbogo alizungumza niaba ya madiwani hao.
Aidha
Mbogo alisema wanawalaani vikali baadhi ya watu ambao wanaobeza jitihada
zinazofanywa na rais za kulinda rasilimali zetu za
nchi na hasa madini kwa ajili ya manufaa
ya Watanzania wote.
Alisema
madiwani wa Manispaa ya Mpanda wanaamini mapato hayo
yatakayopatikana yataongezeka Serikalini na halmashauri
zote zitaongeza uwezo wa kuwahudumia wananchi.
Kwa
upande wake diwani wa Kata ya makanyagio Haidari Sumry aliomba
jitihada za rais zisiishie kwenye madini tu bali nguvu iongezeke kwenye
maeneo mengine iliuchumi wa nchi ukue na
kuongezeka zaidi ya hivi sasa.
Alisema
endapo rasilimali za nchi zitasimamiwa vizuri halmashauri zitanufaika na mapato
yataongezeka Serikalini kwani hata huduma kwenye
halmashauri zitaboreshwa zaidi.
Naye
diwani wa viti maalumu katika halmashauri
hiyo Getruda Kabinda alisema watu waliokuwa wakinufaika
peke yao na rasilimali za nchi ndio wanaobeza na kupinga
jitihada zinazofanywa na rais kwa manufaa ya watanzania wengi katika
kulinda rasilimali za nchi.
Alimuomba
rais Magufuli kukaza uzi kwani watanzania wanyonge wanatambua anachokifanya na
kamwe asikatishwe tamaa na wasaliti wachache kwa maslahi yao,kwani hatua
anazochukua japo siku moja atakufa lakini atabaki anaishi katika mioyo ya
wanyonge Kama baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments