DAKTARI MTANZANIA AFUTWA KAZI NA MADIWANI
Daktari mmoja wilayani Kisarawe amefutwa kazi baada ya kukutwa na
makosa mbalimbali yanayotia hofu juu ya utendaji kazi katika majukumu yake ya
kila siku.
Uamzi huo wa kumfuta kazi Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mtakayo
Emmanuel Shumbusho,umefikiwa na Baraza la Madiwani halmashauri ya
Kisarawe mkoani Pwani.
Dkt Emmanuel Shumbusho anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo
uzembe,utoro kazini ambapo hajaonekana kazini kwa takaribani siku tisa bila
taarifa yoyote kwa mwajiri wake.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamis Dikupatile akitoa maamuzi amesema,wamefikia
hatua hiyo baada ya kubaini mapungufu mengi kutoka kwa mtumishi huyo.
Madiwani wote
kwa pamoja walikubaliana na uamzi huo kutokana na uzembe wa daktari huyo katika
suala zima la utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi na kusababisha kuibuka kwa
usumbufu mkubwa kutokana na kutopatiwa matibabu kwa wakati.
Comments