MUWASA : WAKAZI MANISPAA YA MPANDA WANAKOSA MAJI KUTOKANA NA UPUNGUFU WA MAJI KUTOKA VYANZO VYA MAJI
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
MAMLAKA ya maji safi na salama
Manispaa ya Mpanda MUWASA Mkoani Katavi imesema kuwa,tatizo la upatikanaji wa
maji lililopo kwa sasa kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda,linatokana na upungufu
wa kina cha maji katika vyanzo vinavyotoa maji.
Ikorongo Namba 2 chanzo cha Maji Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) |
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa maji
Mkoani Katavi Mhandisi Zacharia Nyanda wakati akijibu hoja za madiwani katika
kikao cha baraza la madiwani Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda ambacho kimefanyika
katika Ukumbi wa Idara ya Maji Manispaa ya Mpanda.
Mhandisi Nyanda amesema,kwa sasa
kiwango cha maji kinachozaliswa kutoka vyanzo vya maji mbalimbali ni lita za
ujazo Milioni tatu na laki moja na nusu huku mahitaji kwa wananchi yakiwa ni
lita za ujazo Milioni 9.5 ambapo kiasi kinachohitajika kuzalishwa ili kumaliza
tatizo ni lita milioni sita.
Aidha amesema katika kutafuta
ufumbuzi wa tatizo la maji Manispaa ya Mpanda,Mamlaka ya maji safi na salama MUWASA
imekusudia kuongeza lita za ujazo lita milioni moja kwa mwaka huu.
Hata hivyo mbali na wakandarasi
wanaotarajia kuanza mikakati ya kuweka miundombinu ya Maji Manispaa ya
Mpanda,pia Mhandisi Nyanda amesema upo Mpango wa kuvuta maji kutoka ziwa na
Tangamyika na kuboresha chanzo cha maji Ikorongo namba 2.
Miongoni mwa kata ambazo zimetajwa
kukithiri kwa tatizo la maji kwa muda mrefu ni pamoja na kata za Mpanda
Hoteli,Makanyagio,Kashaulili.
Hata hivyo maeneo mengi ikiwemo eneo
la Madukani upungufu wa maji katika vyanzo vyua maji unatokana na mabomba yenye
upana mdogo yanayopitisha maji kutoka vyanzo vya maji hadi kwa wananchi.
Endelea kuhabarika zaidi na P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Mawasiliano kwa ushauri : p5tanzania@g,mail.com
Comments