MKUU WA WILAYA MPANDA AWAAGIZA WATUMISHI WENYE VYETI BANDIA KUJIONDOA WENYEWE KABLA YA KUKAMATWA,MANISPAA YA MPANDA NAYO YAAGIZWA KUWA NA NIDHAMU YA MATUMIZI YA BAJETI YA FEDHA ZA MAENDELEO.
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi. Lilian
Charles Matinga,amewaagiza watumishi wote wenye vyeti bandia Wilayani Mpanda kujiondoa
wenyewe kwa hiari kabla ya kukamatwa na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao.
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga(Asiyevaa wigi) |
Mh.Sebastian Mwakabafu Diwani wa kata ya uwanja wa ndege katika kikao akiuliza swali |
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo leo
katika kikao cha baraza la madiwa Manispaa ya Mpanda ambacho kimefanyika katika
Ukumbi wa Halamshauri ya Manispaa ya Mpanda.
Licha ya kuwa Mkuu wa Wilaya hakutaja
idadi ya watumishi wenye vyeti badia Wilayani Mpanda,Bi.Matinga amesema mpaka
sasa wakati zoezi la ukaguzi likiendelea kuna baadhi ya watumishi wenye vyeti
bandia wamekwishainika.
Hivi karibuni serikali iliagiza nchi
nzima kupitisha msako wa kuhakiki vyeti vya watumishi wote wa umma wenye vyeti
bandia ili waondolewe katika utumishi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya
ametoa agizo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuwa na nidhamu ya matumizi
ya fedha za bajeti kwa ajili ya maendeleo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa
kila bajeti inapopangwa.
Amesema kuwa ni lazima matumizi ya
fedha za serikali yazingatiwe kwa kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya
maendeleo ya wananchi.
Wakati huo huo amesema kila mtumishi Wilayani
Mpanda anatakiwa kuepuka vitendo vya
rushwa,kutouza mali za raia kujinufaisha mwenyewe kwa kivuli cha kuwa kiongozi huku
pia watumishi wakitakiwa kuzingatia mipaka ya mamalaka ya majukumu yao kuepusha
mwingiliano wa majukumu kati ya idara moja na nyingine.
Kikao cha leo ambacho ni cha kwanza
kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kimehudhuriwa pia na Mbunge wa jimbo la Mpanda
Kati Mh.Sebastian Simon Kapufi na Mbunge
viti maalum mkoani Katavi Mh.Rhoda Kunchela.
Endelea kuhabarika zaidi na P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments