MANISPAA YA MPANDA BADO IMESHINDWA KULIPA SHILINGI MILIONI 321 KWA WAZABUNI WALIOJENGA MAABARA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA MANISPAA.
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda Mkoani
Katavi imesema bado haina uwezo wa kulipa Shilingi Milioni 321 inayodaiwa za wazabuni
waliojenga maabara katika Shule Mbalimbali za Manispaa ya Mpanda.
Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Francis Nzungu(PICHA NA.Issack Gerald) |
Katika picha ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Ofisi Za Hamlshauri ya Manispaa ya Mpanda na pia ndipo ulipoUkumbi wa Mikutano wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) |
Ufafanuzi huo umetolewa na Mkurugenzi
Mtendaji Manispaa Bw.Michael Francis Nzyungu wakati akijibu hoja za madiwani
walitaka kujua kiasi cha fedha ambacho Manispaa ya Mpanda inadaiwa na wazabuni.
Bw.Nzungu amesema pia kuwa Kwa sasa
Manispaa ya Mpanda bado haina uwezo wa kulipa fedha za wazabuni hao ambapo hata
hivyo amesema ili kuweza kuwalipa wazabuni itabidi mapendekezo ya uendelezwaji
wa baadhi ya miradi usitishwe ili fedha ambayo ingetumika katika miradi hiyo
itumike kuwalipa waliojenga maabara.
Wakati huo huo amesema kwa sasa uwezo
ulipo ni wa kuwalipa wanaodai kiwango kidogo cha fedha ambapo ametolea mfano
kuwa ni pamoja na makampuni ya ulinzi na vibarua wadogowadogo.
Endelea kuhabarika zaidi na P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Mawasiliano kwa ushauri : p5tanzania@gmail.com
Comments