UKOSEFU WA FEDHA,WAZEE KATAVI WASHINDWA KUHUDHURIA MAADHIMISHO YA KESHO SIKU YA WAZEE DUNIANI YATAKAYOFANYIKA MKOANI MBEYA
Na.Issack Gerald Bathromeo mashama-Katavi
UMOJA wa wazee Mkoani Katavi
umeshindwa kupeleka wawakilishi katika maadhimisho ya Siku ya wazee Duniani
yanayotarajiwa kufanyika kitaifa kesho Mkoani Mbeya.
Moja ya mikitano iliyokuwa ikijadili maslahi ya wazee(PICHA NA Issack Gerald )Septemba 2014 |
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa
Umoja huo Mkoa Bw.Benard Sangija na katibu wa Umoja huo Bw.Marius Bagaya,
wakati wakizungumza na Mpanda Radio katika Ofisi ya umoja huo ziliyopo Mpanda
Mjini.
Kwa mjibu wa Umoja huo,Halmshauri tano
za Mkoa wa Katavi zimetoa taarifa katika umoja huo kuwa,mwaka huu Halmashauri
hazina fedha kuwawezesha wazee kwenda kushiriki maadhimisho ambapo pia mwaka
2015 Halmshauri zilishindwa kufanya hivyo.
Wakati kesho ikiwa ni siku ya wazee
Duniani,Katika Mkoa wa Katavi baadhi ya wazee Manispaa ya Mpanda akiwemo
Bi.Fatma Saleh Mkazi wa Kata ya Majengo(64) wamesema, matatizo makubwa
yanayowakabili na kuwa tishio kwa wazee ni pamoja na suala la ukosefu wa maji
hali inayowapa shida kubwa sana ikiwa hawana nguvu ya kugombania maji na vijana
wenye nguvu.
Mbali na suala la maji, wamesishauri Halmshauri
ya Maniaspaa ya Mpanda kuongeza juhudi za kuzoa taka ambazo kwa sasa wamesema
zimelundikana katika makazi yao na kuhofia kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo
Kipindupindu wakiongeza kuwa kutozolewa taka,Halmashauri inakuwa haijaunga
mkoano ipasavyo juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John
Pombe Magufuli anayetaka Tanzania iondokane na kuzagaa ovyo kwa uchafu.
Katika hatua nyingine,baadhi ya wazee
Mkoani Katavi wameonekana kusikitishwa na hatua ya kustaafu kwa Daktari Patrick
Mwita kwa mjibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma,wakisema kuwa hawana
matumaini ya kupata daktari mwenye upendo kwa wazee kama daktari Patrick ambaye
alikuwa akiwahudumia wazee ipasavyo katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda katika
huduma zinazowalenga wazee.
Wakati huo huo wazee wamesema baadhi
ya ahadi zilizokuwa zimeahidiwa katika maadhimisho ya mwaka 2014 yaliyofanyika kitaifa
mkoani Katavi ilikuwa ni pamoja na wazee kupewa eneo la ujenzi wa Ofisi za
wazee Mkoani Katavi,kupewa pensheni ili kujikimu na maisha ambapo mpaka sasa
ahadi hizo wamesema hazijatekelezwa na kutokana na hali hiyo,wameiomba serikali
kuwaangalia namna ya kuwasaidia wazee hao.
Hata hivyo miongoni mwa mafanikio
makuu baada ya maadhimisho ya mwaka 2014 Mkoania Katavi ni pamoja na wazee
kupewa kipaumbele katika suala la matibabu,kuboreshwa kwa wizara ya afya kutoka
Wizara ya afya na ustawi wa jamii miaka ya zamani na kuwa Wizara ya
afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia wazee na watoto.
Katika sensa ya mwaka 2012 ya watu na
makazi,Mkoa wa Katavi ulibainika kuwa na jumla ya wazee wapatao 5000 ambapo
mpaka sasa jumla ya mabaraza 20 ya wazee katika maeneo mbalimbali ya Mkoani
Katavi yameundwa.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa ya
Tanzania bara ambayo kitaifa iliwahi kuandaa maadhimisho ya siku ya wazee
duniani yaliyoadhimishwa Oktoba mosi mwaka 2014 Wilayani Mpanda.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments