MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AONGOZA HARAMBEE KUWACHANGIA WAATHIRIKA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA SHILINGI MIL.4,656,500 ZAPATIKANA.
NA.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika Katavi
MKUU wa Wlaya ya Tanganyika
Bw.Saleh Mbwana Mhando ameongoza harambee ya kuwachangia waathirika wa
tetetmeko la ardhi Mkoani Kagera ambapo Shilingi MIL.4,656,500/=zimepatikana
ambapo kati ya hizo shilingi MIL.4,416,000/= ni fedha taslimu.
Katika harambee hiyo ambayo imefanyika jana,mkuu wa Wilaya ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya maafa ya Wilaya,mbali na kuwapongeza waliojitokeza kuchangia mchango huo pia ametoa wito kwa wakazi Wilayani Tanganyika kuendelea kuwa na moyo wa kuchangiana katika matatizo.
Kwa upande wa Halmshauri ya
Wilaya ya Tanganyika kupitia kwa Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Mh.Hamad Hassan
Mapengo imechangia shilingi milioni mbili.
Miongoni mwa Idara katika Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika ambazo zimechangia ni Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambayo imechangia Shilingi 272,000/=,Idara ya Mipango Shilingi 38,000/=,Idara ya Mifugo Shilingi 22,000/=,Idara ya Maji Shilingi 47,000/=,Idara ya kilimo,ushirika na umwagiliaji Shilingi 52,500=,Idara ya ujenzi Shilingi 58,000/=,Idara ya elimu Shule za msingi shilingi 73,000/=,Idara ya elimu Sekondari shilingi 110,000/=,Idara ya afya Shilingi 70,000/=.

Idara nyingine ni maendeleo ya
Jamii Shiligi 60,000/=,Idara ya fedha na biashara 38,000/=,Idara ya uchumi na
utawala shilingi 290,000/=,Kitengo cha sheria 15,000/=,Kitengo cha manunuzi
kimechangia 72,000/=,Kitengo cha ukaguzi wa ndani Shilingi 30,000/=,Kitengo cha
kudhibiti ubora wa shule shilingi 54,000/=,TSD Shilingi 28,000/=.
Kwa upande wa michango kutoka
kata 8 kati ya 16 zilizopo Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika ni Shilingi
759,550/= huku kata ambazo zipo katika mchakato wa ukusanyaji michango
zikitegemewa kuwasilisha muda wowote kutoka sasa.
Kata ambazo zimewasilisha michango ni pamoja na Kata ya Mnyagala Shilingoi 41,000/=,Karema 183,050/=,Kabungu 59,500/=,Kasekese 100,600/= Kapalamsenga 64,700/=,Ikola 101,000/=,Isengule 31,000/=,Mpanda ndogo 172,700/=.

Kata ambazo zimesema
zimekwishakusanya na zipo kweny harakati ya kusalilisha ni Mwese Shilingi
109,200,Tongwe 91,300/=,Bulamata 40,000/=.
Aidha kata za
Sibwesa,Katuma,Mishamo,Ilangu na Ipwaga zinaendelea na ukusanyaji mchango.
Hata hivyo Mwenyekiti wa wa
Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Mh.Hamad Hassan Mapengo amesema Halmshauri
ya Wilaya ya Tanganyika haina historia ya kukumbwa na majanga mbali na miaka ya
hivi karibuni nyumba tatu kuezuliwa na upepo na kuharibu mali na makazi ya kaya
tatu Katika kata ya Mpanda ndogo ambapo kamati ya maafa ya Wilaya ya
Tanganyika(zamani MPanda) ikitoa msaada wa Shilingi laki tatu kwa kila mmoja.
Jumla ya Idara 12 za vitengo 5
vya Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika zimeshiriki katika harambee hiyo mbali
na taasisi na watu binafsi ambao nao wameshiriki kwa kuchangia shilingi laki
tatu.
Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera
lilitokea septemba 10 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu na kuleta
uharibifu wa makazi ya watu,shule na vituo vya huduma za afya.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni,ushauri au ukiwa n
ahabari yoyote,tutumie kupitia email ya Ofisi p5tanzania@gmail.com
Comments