MATATIZO MENGI BADO SOKO KUU LA WILAYA YA MPANDA
NA.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika Katavi
SOKO kuu la Mpanda,mkoani Katavi
linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo msongamano wa wafanyabiashara,
mpangilio holela na ukosefu wa taa za kusaidia ulinzi.
Mwenyekiti wa soko hilo Amani Mahela
amesema kuwa ongezeko la wafanyabiashara ndio chanzo cha msongamano, huku
akisema ukosefu wa taa sokoni hapo umesababisha hali ya usalama kupungua na
hivyo kuwafanya walinzi kufanya kazi katika
mazingira magumu.
Katika
hatua nyingine Mahela amesema kuwa soko hilo halina sehemu maalum ya kukusanyia
uchafu hali inayosababisha uchafu kulundikana karibu na maeneo ya biashara kitu
ambacho sio salama kwa watumiaji wa soko hilo.
Hata
hivyo si mara ya kwanza hali ya uchafu katika soko kuu la Wilaya ya Mpanda
kulalamikiwa kwa uchafu kukithiri mahali hapo ambapo pia Halmshauri imekuwa
ikisema kulundikana kwa uchafu kwa muda mrefu kunatokana na uhaba wa magari ya
kuzoa taka na kuzipeleka nje ya Manispaa ya Mpanda.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni,ushauri au ukiwa n ahabari yoyote,tutumie
kupitia email ya Ofisi p5tanzania@gmail.com
Comments